SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 30, 2010

JK ajibu maswali LIVE kwenye TV jana usiku!
Usiku wa jana mgombea urais kwa tiketi ya ccm, Dk, Jakaya Mrisho Kikwete, ameongea na vyombo vya habari vya televisheni, ITV, Channel Ten, TBC1, ATN, Mlimani TV, Star TV na Clouds TV na kuulizwa maswali kadhaa, yakiwemo haya yafuatayo na majibu yake:


TAFITI ZA SYNOVET NA REDET
CCM haina uhusiano na kampuni hizo za utafiti. Synovate wanalipwa na wazungu, Redet pia wanalipwa na wazungu. Sisi pia hatukubaliani na tafiti zao, hatukubaliani na asilimia 61 ya Synovate wala 71 ya Redet, tunaamini tutapata zaidi ya hapo.
Ccm haichakachui matokeo, wanaochakachua mnawajua. Mmeona nao wameanzanisha ya kwao, ambapo baadhi ya viongozi wao wa chama ndiyo wamiliki wa hiyo kampuni ya utafiti…..kicheko…

SUALA LA JIRA KWA VIJANA 
Ukosefu wa ajira ni ‘time bomb’ , lengo limevukwa kwa kuwa na ajira mil 1.3 badala ya mil 1. Hata hivyo mafanikio hayo ni sawa na toni la maji baharini. Bado kuna tatizo la ajira. Tunahitaji wawekezaji ili kupata ajira zaidi na haiwezekani kuwakataa wawekezaji tukawa na ajira. Siri ya ajira ni uwekezaji, hata kama ni mdogo kiasi gani.

SURA YA SERIKALI IJAYO 
Dhamira yangu Kubwa ni kuona tunatumia teknolojia ya mawasiliano zaidi na kuondoa ile tabia ya kufanya jambo lazima ukamuone mtu. Mfano kuomba passport na leseni ya biashara muomboji hatolazimika kumuona ofisa na pia rushwa itapungua.
Pia ifikapo Juni 2011, Wilaya zote zitaunganishwa kwenye mtandao kupitia mkonga wa mawasiliano wa fibre optic. Hivyo sura ya serikali ijayo ni ya e-goverment ambayo itaunganisha wizara zote kwenye mtandao.

UTAPENDA WATANZANIA WAKUKUMBUKE KWA LIPI UKIPATA NAFASI YA KUONGOZA KWA MIAKA MITANO TENA NA KUIMALIZA (LEGACY)
Watanzania wanikubuke kwamba ‘niliwakuta hapa, nimewaacha hapa’ basi! Niliwakuta wakiwa hali ya chini na nimeondoka wakiwa na nafuu. Hii ikiwa ni katika kila sekta zote, barabara, elimu, afya, n.k.

VITAMBULISHO VYA URAIA VP? HILO LIMEKWAMA WAPI NA KAMA HALIJAKWAMA LIMEFIKA WAPI?
Ni kweli kwamba ahadi ya vitambulisho ni ya muda mrefu, siyo la awamu hii tu. Bahati mbaya sana ni mradi ambao umepitia misukosuko mingi na imechangiwa na migongano ya kimaslahi ya watu binafsi. Hata hivyo baada ya muda atapatikana mtu wa kufanyakazi hiyo, katika miaka miwili ijayo vitakuwa vimetoka au vitakuwa vimeenza kutoka.

SEKTA YA MADINI SERIKALI IMECHUKUA HATUA GANI BAADA YA KUUNDA KAMATI?
Tumetengeneza sera na sheria mpya ya Madani. Tumerekebisha viwango vya mrabaha, kuna maeneo tumeongeza na maeneo mengine tumepunguza. Una manufaa ya pande zote. Wa Mwanzo ulikuwa umetulalia sisi, lakini sasa mchango wa Madini umeanza kutoa mchango mkubwa wa mapato. Kwa mwaka huu umeingiza zaidi ya dola milioni 4.5

WATU WENGI WANAPELEKWA NJE KWA MATIBABU!
Tunalazimika kupeleka watu wetu nje kwa sababu bado baadhi ya mardhi hatuna uwezo wa kuyatibu. Tunapeleka watu nje kwa sababu hatuna wataalamu au vifaa vya kutibu maradhi hayo. Katika kipindi hiki, tumefundisha madaktari wapatao 265 kutoka 46.
Tumejenga pale Muhimbili kitengo cha kutibu magonjwa ya kinywa ambacho ni bora kuliko vyote Afrika Mashariki na kati. 
Pia tumeshaweka jiwe la msingi katika hospitali ya Muhimbili la kujenga kitengo cha kutibu magonjwa ya moyo (open surgery) ambacho kitakuwa na vitanda 100.
Tumejenga mashine ya kusafisha figo Muhimbili, ambayo ina vifaa vyote vya kisasa (complete equipment), hii yote ni kuhakikisha tunakuwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengi hapa hapa nchini.
Pia kitengo cha MOI kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya upasuaji wa misuli kuanzaia mwakani.

MUUNGANO: KUNA TATIZO LA MUUNGANO, UNAWEZA KUTUPA SURA YA SERIKALI YA MUUNGANO INAYOKUJA ILI KUONDOA MALALAMIKO.
NI kweli kila wakati kuna maswali yanaibuka kuhusu muungano. Lakini kuna kamati maalum imeundwa kushughulikia suala la muungano na matatizo mengi yameshatatuliwa na kuna masuala mengi tumekubaliana. Masuala yaliyobaki kujadiliwa ni machache ambayo katika kipindi kijacho yote tutakuwa tumeyapatia majibu.

UMETOA AHADI NYINGI SANA NA TAMU SANA, JE AHADI HIZI ZITATEKELZWA VP?
Kwanza kuna ilani za chama na kuna ahadi za papo kwa papo. Katika awamu ya kwanza mara baada ya cunda serikali, nilikutana na mawaziri wote, nikawapa ilani na kuwataka kuandaa mpango wa utekelezaji wa ilani zilizotolewa na nyingi zimetekelezwa. Tunakutoa wasiwasi, mengi ya haya tunayoyaahidi tutayatekeleza.

UTASHUGHULIKIA VP SUALA LA RUSHWA
Kwanza tumetunga sheria ya kupambana na rushwa na baada ya hapo tumejenga taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, TAKUKURU, tumeiongezea uwezo. Kwa kufanya hivyo matokeo yake tumeyaona, wameweza kuwafikisha watu wengi mahakamani. Lakini tatizo la rushwa ni Kubwa hata katika vitabu vya dini limetajwa. Nawaahidi tutaendelea kupambana nalo.

MANUNG’UNIKO DHIDI YA MAHAKAMA
Tumeanza kujenga mfumo wa kisasa wa kusikiliza kesi ambapo mienendo yake itakuwa ikirekodiwa kama hansard. Pia tumeongeza majaji, kuna tatizo la maadili kwa watendaji, hili tunaomba tushirikiane kulitatua.

MWISHO
RAI YA RAIS: TUENDELEE KUDUMISHA AMANI, TUHESHIMU MATOKEO. TUMIENI KURA ZENU KUMCHAGUA MNAYEMTAKA. TUSICHAGUANE KWA MISNGI YA DINI. VYOMBO VYA HABARI VIACHE KUCHOCHEA MAMBO.
chanzo http://www.globalpublishers.info/

0 comments:

Post a Comment