SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 30, 2010

Uchaguzi mkuu kufanyika kesho Tanzania
Raia wa Tanzania wanajiandaa kwa uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika hapo kesho.
Wafuasi wa chama cha CCM
Wafuasi wa chama cha CCM
Vyama vya kisiasa vinatarajiwa kukamilisha kampeini zao hii leo.
Wafuasi wa rais wa nchi hiyo, Jakaya Kikwete wanatarajiwa kufika jijini Dar es Salaam, kuhudhuria mkutano wa mwisho wa kampeini,wa chama tawala cha CCM.
Kuna ushindani mkali katika kinyanganyiro cha kuwania kiti cha urais.
Miongoni mwa watu wanaowania kiti hicho ni pamoja na rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alizoa asilimia 85 ya kura zote zilizopigwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete
Wakosoaji wa Rais Kikwete wanasema ameshindwa kukabiliana na ufisadi na kuhakikisha kuwa rasilimali ya nchi inawafikia raia wa Kawaida.
Rais Kikwete atapamabana wapinzani wengine akiwemo Willibrod Slaa ambaye ameahaidi kupambana na ufisadi na kuanzisha huduma za afya na elimu bila malipo nchini humo endapo atachaguliwa kuongoza taifa hilo.
Mwingine ni Ibrahim Lipumba ambaye amehaidi kubuni serikali ya muungano wa kitaifa ili kutatua matatizo ya taifa hilo ikiwa atashinda uchaguzi huo.
Wapiga kura milioni 19.6 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo.


Tunamuomba M/Mungu ajaalie Uchaguzi huu ufanyike mwanzo hadi mwisho uwe wa Haki na Huru, Salama na Amani.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Amin.

0 comments:

Post a Comment