Ivory Coast kuandaa uchaguzi mkuu kesho
Rais wa Ivory Coast
Raia wa Ivory Coast wanajianda kwa uchaguzi mkuu utakaoandaliwa hapo kesho, uchaguzi ambao ni wa kwanza kwa zaidi ya miaka 10.
Inatarajiwa kuwa uchaguzi huo mkuu utaunganisha tena taifa hilo ambalo liligawanyika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.
Tangu wakati huo sehemu kadhaa za taifa hilo zimekuwa chini ya uthibiti wa makundi ya waasi.
Rais wa sasa Laurent Gbagbo, atapambana na rais wa zamana wa nchi hiyo Henri Konan Bedie, ambaye aliondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi mwaka 1999.
Mgombeaji mwingine ni Alassane Outtara ambaye hakushiriki katika uchaguzi zilizopita kwa kuwa alituhumiwa kuwa raia wa kigeni.
Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanasema uchaguzi huo utakuwa mgumu na huenda asipatikane mshindi wa moja kwa moja.
Vile vile wanaonya kuwa huenda ghasia zikashuhudiwa nchini humo ikiwa matokeo ya uchaguzi wa urais yatakuwa na utata
0 comments:
Post a Comment