SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, January 7, 2014

TAARIFA YA KUAHIRISHWA KWA SAFARI YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA YA LEO JUMANNE JANUARI 07, 2014 HADI KESHOKUTWA ALHAMIS JANUARI 09, 2014!

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka leo Jumanne Januari 07, 2014 saa 3 usiku kwenda bara imeahirishwa hadi keshokuwa siku ya Alhamis Januari 09, 2014, saa 3 usiku.

 Taarifa hiyo imefafanua kuwa dharura hiyo ya kuahirisha safari imetokana na ajali ya treni ya mizigo iliyotokea juzi saa 2 usiku kati ya Stesheni za Luiche na Kigoma na kusababisha treni ya abiria kutoka Kigoma kushindwa kuondoka kuja Dar. 

 Wakati huo huo taarifa iiliyopatikana mchana huu imethibitisha kuwa ukarabati wa eneo lililoathirika na ajali ya treni ya mzigo ya juzi umekamilika na njia imefunguliwa saa 8:45 mchana huu. Aidha treni ya abiria kutoka Kigoma kuja Dar imeshaondoka mjini Kigoma tokea saa 9:20 alasiri ya leo. 

 Aidha taarifa hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

 Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji 
 Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu. 
 TRL Makao Makuu, 
 Dar es Salaam. 
 Januari 07, 2014

0 comments:

Post a Comment