Misri yawakandamiza wapinzani na kukataa wasimamizi wa nje
Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imeelezea wasiwasi wake kuhusiana na vitendo vinavyoongezeka vya serikali vya kuwakandamiza wafuasi wake, kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Mohammed Badie Kiongozi wa harakati hiyo ametoa matamshi hayo huku polisi ya Misri ikiwa mpaka sasa imewakamata zaidi ya wafuasi 250 wa harakati hiyo mwezi huu. Ikhwanul Muslimin inahesabiwa kuwa ni chama cha upinzani chenye nguvu na tishio kwa chama tawala katika uchaguzi ujao wa bunge nchini humo.
Wakati hayo yakiripotiwa, chama tawala cha Misri kimekataa kuwepo aina yoyote ya wasimamizi kutoka nje ya nchi katika uchaguzi ujao wa bunge wa nchi hiyo. Zakaria Azami Naibu Katibu wa chama hicho anayesimamia masuala ya fedha na ya kiidara amesema kuwa, chama hicho hakikubaliani na kuwepo aina yoyote ya usimamizi wa kimataifa katika uchaguzi wa bunge na hivi karibuni kitatangaza rasmi wagombea wake.
chanzo http://kiswahili.irib.ir/
chanzo http://kiswahili.irib.ir/
0 comments:
Post a Comment