Wafanyakazi wa WCF wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuruwakati wa matembezi ya kilele chasiku ya wafanyakazi Duniani
Matembezi yakipita barabara ya Chang’ombe
Matembezi yanaendelea, hapa ni barabara ya Uwanja wa Taifa mkabala na ofisi za TAKUKURU wilaya ya Temeke
Matembezi yakiendelea barabara ya Chang’ombe
Matembezi yakiendelea barabara ya Chang’ombe
Baadhi ya wafanyakazi wa
WCF, wakimsikiliza mwenzao aliyevaat-shirtyenye ujumbe maalum wa Mfuko
huo “WCF inatoa Fidia Stahiki kwa Wafanyakazi wote wa Sekta ya Ummana
Binafsi”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar
esSalaam, Mh. Paul Makonda, (kulia), akiteta jambo na kiongozi wa
Shirikisho la Wafanyakazi mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kilele cha
May Day uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa
WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha matembezi hayo
kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa
WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha matembezi hayo
kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa
WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha matembezi hayo
kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
MFUKO wa
Fidia Kwa Wafanyakazi, WCF, kwa mara ya kwanza umeshiriki kwenye
matembezi ya kusherehekea siku ya Wafanyakazi, maarufu kama MAY DAY
jijini Dar es Salaam leo Mei 1, 2016.
Matembezi hayo
yaliyoshirikisha wafanyakazi kutoka sekta ya Umma na Binafsi, ambazo
ndio wadau wakubwa wa Mfuko huo, yalianzia kwenye ofisi za Shirikisho la
Vyamavya Wafanyakazi, TUCTA, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kupita
barabara ya Nkurumah, Nyerere
na
kisha kupinda barabara ya Chang’ombe hadi uwanja wa Uhuru
ambako yalipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda.
WCF ni
Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa
mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi
namba 20 ya mwaka 2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa
mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.
Tangu kuanzishwa
kwa Mfuko huo, juhudi za kutangaza hudumazake kwa wadau
zimekuwa zikiendelea mfululizokwa kutoa elimu kupitia semina,
maonyeshona makongamano lakini pia kupitia vyombo vyahabari na kwa siku
ya Mei Day imekuwa ni fursa kubwa ya WCF kuungana na wadau wake wakubwa.
Baadhi ya
wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki
matembezi ya kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani (May day), hapa
matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2016.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
0 comments:
Post a Comment