SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, January 15, 2014

MAGARI MAWILI YAWAKA MOTO IRINGA WAKATI WANAFUNZI WA WELDING WAKIJIFUNZA KUUNGA NGAO

Wananchi Iringa  mjini  wakilitazama daladala  lililowaka  moto wakati likiwa kwa mafundi welding  likichomelewa leo eneo la uwanja wa  samora


Daladala  likiwaka  moto  huku kikosi cha zimamoto na uokoaji  wakizima moto huo
Gari la Zimamoto na uokoaji mjini Iringa likizima moto  uliokuwa ukiteketeza daladala eneo la Samora  leo
Hili ni basi  ambalo pia  limewaka upande wa mbe
Konda  wa daladala  hilo akiwa na kifaa cha kuzimia moto ambacho  kimenusurika katika moto  huo
Mmoja kati ya askari wa  Zima moto mjini Iringa akilitazama daladala  hilo
Hivi  ndivyo  moto huo  ulivyoteketeza daladala  hilo
Askari  wa kikosi  cha  Zimamoto na uokoaji mjini Iringa Bw  JOhn Zacharia akikagua kifaa cha  kuzimia moto ambacho kilikutwa  kikiwa  kibovu na si msaada  kwao
Bw Filibert Mwihava  akizungumza na mtandao  huu
Huyu ni mmoja kati ya mafundi  wazoefu ambao  walikuwa  wamewaachia  wanafunzi hao kazi
Na Francis Godwin 
BASI mmoja lanusurika  kuwaka  moto na daladala  moja  yateketea yote kwa moto  wakati  wanafunzi wa masomo ya  kuunga vyuma katika gereji  bubu  eneo la uwanja  wa  Samora  mjini  Iringa  wakijifunza kuunga ngao  ya  daladala  hiyo yenye  namba za  usajili T189 AWN .

Tukio  hilo  limetokea  leo majira ya 2.15 mchana  wakati  vijana  wawili wanaojifunza  kuunga  wakiendelea na  mafunzo ya  kuunga  ngao ya  daladala  hilo.

Akizungumzia ajali  hiyo mmoja kati ya  wafanyakazi wa gereji  hiyo Filibert Mwihava  alisema  kuwa chanzo  cha  daladala  hilo  kuwaka  moto ni  vijana  wawili ambao  wanajifunza  ufundi  wa  kuunga  vyuma katika eneo hilo kufanya  kazi  hiyo  bila kuzingatia kanuni ya kazi hiyo.

Kwani  alisema  vijana hao  walikuwa  wakiunga ngao ya nyuma ya  daladala  hilo jirani na tenki la mafuta  na kutokana na cheche  zilizokuwa  zikitoka  zilisababisha moto kuibuka kwa kasi .

Hata  hivyo  alisema mbali ya  kuwa na kifaa cha kuzimia  moto  bado walishindwa kukitumia  kifaa hicho  kutokana na kutokuwa na elimu ya  kutosha  ya kukitumia.

Mwihava  alisema kutokana na moto  huo kushika daladala  hilo linalofanya  safari  zake kati ya  Tumaini na Zizi la Ng'ombe  mjini  Iringa hakuna mtu  aliyezulika  zaidi ya  basi  lenye namba za  usajili T 457 AMQ kutetekea  upande wa  mbele  kabla ya  kuokolewa .

Pia  alishukuru  kikosi cha  zimamoto  na uokoaji mjini Iringa ambao  walifika kwa  wakati na kufanikiwa  kuzima moto  huo ambao  ungeweza  kusababisha  madhara  makubwa katika  eneo hilo ikiwa ni pamoja na ofisi  maduka  ya  watu  waliojenga  kuzunguka uwanja  wa  Samora  kuteketea..

Akithibitisha  kutokea  kwa  tukio  hilo kiongozi  wa askari wa zimamoto  ambao  walifika  eneo hilo John Zacharia  alisema  kuwa  kuwa  chanzo cha moto  huo ni uzembe wa ofisi  hiyo.

Kwani  alisema hata  kifaa cha zimamoto  walichokuwa  nacho kilikuwa hakifanyi kazi kutokana na kuharibika muda mrefu.

Huku  kifaa cha  kuzimia  moto  kilichokuwemo katika daladala  hilo ni kifaa ambacho  kidogo  zaidi na maalum kwa gari dogo ambacho  pia  kilikuwa hakifanyi kazi.

Zacharia  aliwataka   wamiliki wa  vyombo vya usafiri  kuzingatia sheria  za  zimamoto ya  kuwa na vifaa vya kuzimia  moto badala ya  kudanganya na  kuona kama wanaonewa  pale  wanapolazimishwa  kuwa na vifaa hivyo.

0 comments:

Post a Comment