Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo
Akipokelewa na Viongozi katika kata ya Mtamba Jimbo la Morogoro kusini lililopo
Wilaya ya Morogoro Vijijini alipotembelea Wilaya Hiyo wakati akikagua Mradi wa
Kusambaza Umeme vijijini Mradi Uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo La
MCC.Waziri Muhogo Amesema Serikali ina nia ya kusambaza Umeme Vijiji vyote
tanzania Ili kila mtanzannia afaidi nishati hiyo..
Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo
akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro alipotembelea
wakati akianza ziara yake katika Mkoa wa morogoro.
Katika ziara hiyo waziri Muhongo amesema Serikali ya
CCM Imeamua Kutokomeza kabisa Umaskini na ndiyo maana inasambaza Nishati ya
Umeme kwa kasi kubwa ili Nishati hiyo iwasaidie watanzania katika shuguli za
uchumi ikiwemo Elimu,Viwanda na matumizi Mengine.Aidha Waziri Muhongo Amesema
kuwa Kumekuwa na uharibufu Mkubwa wa Mazingira hali inayoashiria Jangwa kutokana
na uvunaji wa miti kwajili ya Uzalishaji wa Mkaa na wameamua kusambaza Nishati
ya Umeme kwa haraka ili kuiokoa nchi kuwa Jangwa.
Waziri muongo ameongeza kwamba kwa sasa Bei ya
kuwaunganishia wananchi umeme Imeshushwa Mpaka Shilingi 177,000/= tu kwa lengo
la kuwawezesha watanzania wenye pato la chini kuunganisha umeme na kunufaika na
Nishati hiyo.Pia waziri Muhongo ameongeza Shirika la Umeme wameagizwa kupokea
Fedha kidogo kidogo kwa wananchi wote watakohitaji kuunganishiwa umeme na hawana
Uwezo wa Kulipa fedha zote kwa Pamoja..
Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo
Akisaini Kitabu cha wageni kata ya Mtamba wilaya ya Morogoro Vijijini kabla ya
kusikiliza kero za Wananchi wa wilaya hiyo kuhusu Umeme na uchimbaji wa
Madini
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa morogoro ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris Kushoto akiwa na Waziri wa
Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo kulia wakisikiliza taarifa ya Chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Iliyokuwa inasomwa na Katibu wa ccm Mkoa wa Morogoro
hayupo pichani.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Kushoto Akiwa
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro
Kusini Mh Innocent Kalogeris wakati walipompokea waziri wa Nishati na madini Mh
Sospert Muhongo Mjini Morogoro
Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo
Akiuliza jambo kwa Injinia wa shirika la umeme mkoa wa morogoro Ndugu Maro
walipotembelea Kituo cha kuunganishia Umeme kilichopo Pangawe wakati wa ziara ya
Waziri huyo ya Kukagua miradi ya kusambaza Umeme vijijini Mkoani
Morogor
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa morogoro ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris Akifafanua Jambo katika
ziara ya waziri huyo na kushoto ni Meneja Wa Tanesco Mkoa wa Morogoro
Akisikiliza kwa makini
0 comments:
Post a Comment