Waziri wa mashauri ya kigeni wa
Marekani John Kerry amezumgumzia misukosuko inayozidi kuongezeka kusini
mwa bahari ya China alipokutanma na viongozi wa vyeo vya juu wa chama
cha Kikomisti mjini Beijing.
Ameitaka China kuchukua hatua ili
kupunguza misukosuko eneo hilo. Marekani inasema kuwa China imejenga
miradi ya ardhi ya karibu ekari 800 kwenye visiwa vya Spratly mwaka
mmoja uliopita.Nazo meli za jeshi la marekani zimekuwa zikipiga doria kwenye visiwa vya spatry ambavyo vinadaiwa na china na nchi zingne tano.
China inaamini kuwa Marekani inazichochea nchi za Asia kukabiliana nayo katika kudai maeneo ya bahari.
CHANZO: NA BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment