Utafiti huo umebaini kwamba wagonjwa wanaopewa dawa hizo za kupunguza maumivu mwilini kwa mda mrefu wana hatari kubwa ya asilimia 63 kuaga dunia haraka.
Hatari ya kupatikana na ugonjwa wa moyo iko juu kwa asilimia 68 huku pia kukiwa na hatari kubwa ya asilimia 50 ya kupatikana na vidonda vya tumbo ama hata kuvuja damu.
Paracetamol kama zinavyojulikana hupendelewa sana na madaktari wengi wakidai ni salama kushinda Aspirin, ambayo imehusishwa na kuvuja damu tumboni na Ibuprofen ambayo imehusishwa na magonjwa ya moyo na kiharusi.
Lakini watafiti wa Uingereza waliofanya uchunguzi huo uliowahusisha wagonjwa 666,000 wanasema kuwa hatari hiyo huenda ilipuuzwa na sasa wameagiza uchunguzi ufanywe kuhusu usalama wa dawa hiyo.
Wanasayansi hao wanatoka katika taasisi ya matibabu ya Rheumatic and Musculoskeletal iliopo mjini Leeds
0 comments:
Post a Comment