_65680924_006525189-1
Na Mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa idadi ya watoto wanaofikiria kujiua imeongezeka ghafla nchini Uingereza hali inayoonyesha kuwepo ongezeko la asilimia 116 kulinganisha na kesi zilizorekodiwa katika kipindi cha kati ya mwaka 2010 na 2011.
Taasisi ya utoaji huduma za ushauri ya childline imeripoti kuwa imepokea simu 34,000 katika kipindi cha kati ya mwaka 2013 na 2014 za vijana wa kiingereza wenye umri wa chini miaka 18 ambao wamekuwa wakifikiria kujiua.

Karibu vijana wote chipukizi 6,000 walioomba ushauri walikiri kwamba walihawi kutaka kujiua hali inayoonyesha kuwepo ongezeko la asilimia 43 kulinganisha na mwaka uliopita.
Esther-Rantzen-ChildLine-e1340828873746
Mwasisi wa taasisi ya childline Esther Rantzen.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa vijana wenye umri wa miaka 15 ndiyo wengi zaidi kati ya vijana waliopatiwa ushauri katika kipindi cha mwaka huu.
Mwasisi wa taasisi ya childline Esther Rantzen amesema hivi sasa kituo hicho kinapokea simu nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla kutoka kwa vijana wa Uingereza waliokata tamaa kwa simanzi na huzuni.

CHANZO: DEWJI BLOG