Waziri
wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee akifungua
maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es
salaam” na kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi chini ya kauli mbiu isemayo “ Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.
Baadhi
ya wadau mbalimbali na wataalam wa takwimu waliohudhuria maadhimisho ya
Siku ya Takwimu Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda
Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo kuhusu
matumizi ya takwimu sahihi katika kupanga shughuli za maendeleo nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohammed Hafidh akisisitiza jambo kuhusu athari, madhara na ya matumizi ya takwimu zisizo sahihi.
Mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw. Jacques Morisset (kushoto) akizungumza
na wadau mbalimbali kuhusu mchango wa matumizi ya takwimu sahihi katika
maendeleo ya taifa lolote wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu
Afrika leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ferdha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee (wa nne
kutoka kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji na
watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua
maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
*****
MAADIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM, SERIKALI YASISITIZA UWAZI KATIKA TAKWIMU.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO. Dar es salaam.
SERIKALI
kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa itaendelea kuwapatia
wananchi takwimu sahihi zinazohusu sekta mbalimbali ili kuwajengea uwezo
wa kushiriki katika ngazi za maamuzi na masuala mbalimbali nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee wakati akifungua rasmi
maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yanaoongozwa na kauli mbiu isemayo
Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.
Amesema
upatikanaji wa taarifa na takwimu sahihi kwa wananchi unaongeza
ushiriki wao katika maamuzi na kuwajengea uwezo wa kutathmini utendaji
wa Serikali katika masuala mbalimbali yakiwemo mapato na matumizi.
Amesema
Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kuhakikisha kuwa takwimu
mbalimbali zinapatikana kwa urahisi kupitia mtandao, machapisho na
mifumo rahisi ili kuwawezesha wananchi na wadau mbalimbali kuzipata
pindi wanapozihitaji.
“
Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu yanaongozwa na kauli
Mbiu isemayo Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau
wote ambayo inalenga kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi kwa
urahisi na kumwezesha mtumiaji kuzipata bila kizuizi chochote” Amesema.
Amefafanua kuwa
upatikanaji wa takwimu huria unawawezesha wananchi kujua sababu
zinazoifanya serikali kutekeleza maamuzi mbalimbali, kuongeza
uwajibikaji na kuwawezesha kupima matokeo ya sera za Serikali,
kutathimini matumizi ya Serikali na kushiriki katika midahalo mbalimbali
ya kitaifa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bi. Aldegunda Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi hiyo amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu
yameweka msisitizo katika kuweka miundombinu ya kuwarahisishia wadau
kupata takwimu sahihi kwa wakati.
Amesema
maadhimisho hayo licha ya kujadili masuala mbalimbali yanajikita katika
kuweka msukumo wa kuhakikisha kuwa takwimu sahihi zinawafikia wananchi
na wadau mbalimbali wa maendeleo bila vikwazo vyovyote ili kuongeza
uwazi wa utendaji wa shughuli za serikali serikali.
Naye
mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw.Jacques Morisset
akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ameeleza kuwa takwimu sahihi ni
ufunguo wa maendeleo kwa nchi yoyote duniani.
Amesema
kuwa upatikanaji wa taarifa mbalimbali unawawezesha wananchi kutambua
na kupima kiwango cha maendeleo ya nchi yao katika masuala mbalimbali
yanayogusa maisha yao ya kila siku yakiwemo ya matumizi ya rasilimali,
Elimu, ukuaji wa uchumi, shughuli za kilimo na sekta ya viwanda na
Biashara.
0 comments:
Post a Comment