Kivuko
cha MV.Dar es Salaam kikiwa kimeshushwa majini leo tayari kwa kuanza
safari ya kuja nchini Tanzania kutokea nchini Denmark.
ILE ahadi
ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ya kununua Kivuko kipya kwa
ajili ya kutoa huduma ya usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam na
mwambao wa Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo imetimia baada ya kukamilika
kwa Kivuko cha Mv Dar es Salaam.
Imeelezwa
kuwa kivuko hicho cha 'Mv Dar es Salaam' kilichokuwa kikieundwa huko
nchini Denmark, kimekamilika na leo kimegusa rasmi majini na tayari
kinatarajia kuanza safari ya kuja jijini Dar es Salaam ambapo
kinatarajiwa kuwasili katika ardhi ya Tanzania jijini Dar es Salaam
baada ya wiki tatu mpaka nne zijazo kuanzia leo.
Aidha
imeelezwa kuwa kiivuko hicho kitakuwa ni cha kwanza kwa kuwa na kasi
kubwa kuliko kivuko chochote Afrika ya Mashariki na hasa katika Mwambao
wa bahari ya Hindi ukiondoa Afrika ya Kusini.
Kivuko
hiki ni muendelezo wa juhudi za Wizara ya Ujenzi za kupunguza
msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na
kujenga barabara za New Bagamoyo (Kawawa JCT - Tegeta); ujenzi wa
miundombinu ya mabasi yaendayo kasi (Bus Rapid Transit Infrastructure -
BRT).
Pamoja
na kuanza kwa ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo kasi awamu ya
pili ; ujenzi wa ‘Flyover’ ya TAZARA na UBUNGO ; barabara za pete (DSM
Outer Ring Roads); barabara ya Dar es Salaam – Chalinze Express way;
kupanua barabara ya lami sehemu ya Gerezani (KAMATA – Bendera Tatu)
kutoka njia mbili za sasa hadi njia nne; kujenga daraja la Kigamboni
linalounganisha Kurasini na Kigamboni, ambalo linatarajiwa kukamilika
mwezi wa sita mwakani.
Kivuko
cha MV.Dar es Salaam kikiwa kimeshushwa majini leo tayari kwa kuanza
safari ya kuja nchini Tanzania kutokea nchini Denmark.
0 comments:
Post a Comment