SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 26, 2011

WATANZANIA LEO WAFANYA MAADHIMISHO YA MIAKA 47 YA MUUNGANO

Leo ni siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Pichani ni Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere akichanganya mchanga wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe za kuuasisi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete leo amewaongoza watanzania katika kilele cha maadhimisho ya siku ya muungango wa Tanzania yaliyofanyika kitaifa visiwani Zanzibar.
Katika maadhimisho hayo rais Kikwete aliingia katika uwanja wa Amaan visiwani humo akiwa katika gari la wazi, ambalo lilizunguka uwanja huo huku rais kikwete kiwapungia mkono wananchi waliohudhuria.
Baada ya hapo rais aliwenda katika jukwaa maalum ambapo alipigiwa mizinga 21 kwa heshima yake huku wimbo wa taifa ukipigwa na bendi ya polisi.
Rais pia akagua gwaride la heshima na kisha vikosi vya jeshi la ulinzi vilipita mbele yake kwa mwendo wa pole na baadae vilipita kwa mwendo wa kasi.
Sherehe za maadhimisho hayo zimehudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais Mohammed Gharib Bilal na rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dakta ali Mohammed Shein pamoja mabalozi wa nchi mbali mbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania.
MATUKIO PICHANI:
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa Amani Zanzibar(Unguja) leo hii kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa kwenye jukwaa na rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Dr. Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Michezo wa Amaani mjini Unguja kuongoza sherehe za miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia mke wa muasisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa Aman mjini unguja kuongoza sherehe za muungano wa Tanzania na Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akiukagua gwaride lilioandaliwa namajeshi ya ulinzi katika uwanja wa michezo wa Amani wakati wa shrehe za miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Wakuu wakiwa jukwaa kuu
Sehemu ya umati wa wananchi
Umati wa wananchi
Viongozi na mabalozi wa nchi mbalimbali
Halaiki na Paredi.
Picha na Freddy Maro

0 comments:

Post a Comment