Mgodi
wa dhahabu wa Geita Gold Mine uliopo mkoani Geita. Mgodi huu ni moja ya
makampuni yanayowania tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Mshauri
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mine katika masuala ya serikali na
jamii Bw. Clement Msalangi (mbele kwa mbali) akielezea mafanikio ya
mgodi wa Geita Gold Mine katika utoaji wa huduma bora kwa jamii na
uwezeshaji kwa timu ya majaji na sektretarieti iliyofanya ziara katika
mgodi huo.
Meneja
Mahusiano ya Jamii Bw. Manase Ndoloma akisisitiza jambo katika kikao
kilichoshirikisha uongozi wa mgodi wa Geita Gold Mine na jopo la majaji
na sekretarieti kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma
za Jamii na Uwezeshaji iliyotembelea mgodi huo.
Mtaalamu
katika masuala ya mahusiano na maendeleo ya jamii Bw. Joseph Mangilima (
wa pili kutoka kulia) akielezea mchango wa mgodi wa Geita Gold Mine
katika mradi wa maji mbele ya bwawa la Nyankanga ambalo maji yake
yatasafishwa na kusambazwa kwa wananchi wa Geita kupitia ufadhili wa
mgodi huo.
Mtaalamu
katika masuala ya mahusiano na maendeleo ya jamii Bw. Joseph Mangilima (
wa kwanza kulia) akitoa maelezo juu ya mchango wa mgodi wa Geita Gold
Mine katika ujenzi wa kisima mbele ya timu ya majaji na sekretarieti
iliyotembelea mradi huo.
Afisa
Afya Mkuu wa mgodi wa Geita Gold Mine Dkt. Kiva Mvungi ( wa pili kutoka
kulia) akielezea mchango wa mgodi wa Geita Gold Mine katika ujenzi wa
kituo cha upimaji wa virusi vya Ukimwi na utoaji wa ushauri nasaha cha
Geita mbele ya baadhi ya majaji na watendaji wa mgodi huo waliotembelea
kituo hicho.
Meneja
Mahusiano ya Jamii Bw. Manase Ndoloma (katikati) akielezea majaji na
sekretarieti mchango wa mgodi wa Geita Gold Mine katika ujenzi wa nyumba
mpya kwa ajili ya wakazi wa Geita waliohamishwa kwa ajili ya kupisha
shughuli za mgodi huo.
Mtaalamu
katika masuala ya mahusiano na maendeleo ya jamii Bw. Joseph Mangilima (
wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele) akiongoza timu ya majaji,
sekretarieti na wataalamu wengine kutoka mgodi huo katika ziara kwenye
kituo cha watoto yatima cha Moyo wa Huruma, kinachofadhiliwa na mgodi
huo.
0 comments:
Post a Comment