Hizi
ni Chemba mbili ambazo zimesha jaa na Kupasuka na kusababisha uharibifu
mkubwa wa Mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hili la Umoja
street ambapo sasa panaitwa Kinyesi Street.
Majani
Haya si kwamba yamekuwa Kijani kuna mvua katika kipindi hiki cha
Kiangazi lakini ni kwamba Maji machafu yanayo Churuzika kila wakati
ndiyo yamesababisha kuwepo kwa hali hii hatarishi
Unaweza
kudhani kwamba kuna watu wanakuja kufanya kazi ya kuzibua hizi Chemba
hapa , lakini la hasha zimefunguliwa tuu, hii si chemba ya mtu binafsi
lakini ni chemba ya mkondo wa maji Taka.
Hivi
ndivyo inavyo onekana Moja ya Chemba katika mtaa huu.. Chemba hii
inakaribia kabisa kujaa na ikisha jaa itasababisha Madhara makubwa sana
katika eneo hili, Tayari chemba mbili zimesha fumuka,Kama takataka
zinavyo onesha kwamba muda wowote zikiziba basi chema hizi zitaachia na
kuanza kumwaga maji hayo machafu. hii imepita ukutani kwa mtu mda wowote
inafumuka
Picha
inajileza yenyeww hapa Tazama majani yalivyo stawi vizuri sana, Tazama
chemba hii ilivyo kaa muda mrefu mpaka inaelekea Kuoza sasa, ni moja ya
chemba ambayo kwanza haina mfuniko jambo ambalo ni hatari, pili ni la
maji machafu ambayo yanaweza sababisha magonjwa ya mlipuko. Hii ni
chemba sugu
Hali
hii ndiyo iliyo sababisha mtaa huu kuitwa Kinyesi Street, kwa mbali
kuna mkazi wa eneo hili anaonekana kuvuka barabara kwa shida sana jambo
ambalo linaonesha mtaa mzima hasa eneo hili pamejaa maji taka .
Hii
ni Chemba ya Maji Taka ambayo kwa msingi kabisa inamwaga maji mengi
sana kwa kai ya ajabu pia , mkondo huu ambao sasa umesemwa mpaka
wananchi wameamua kunawa mikono na kukubaliana na mtaa wao kuitwa
Kinyesi Street.
Hili
ni eneo Hatari sana Hapa Chemba imefumuka inamwaga maji utazania ni
yanatoka katika chanzo cha mto, hali hii ni hatarishi sana
Picha
inaelezea Uhalisia kabisa wa Jambo ... Tazama jinsi majani ya upande
kwa kulia yalivyo stawi , tazama ya upande wa kushoto yote ni kutokana
na Maji taka.
Mbaya
zaidi wakati Chemba moja inatema maji kwa wingi hii ipo Jirani kabisa
ambapo ukitazama picha ya kwanza ndipo utaelewa vizuri sana . chemba
hizi ni hatari sana na mpaka sasa zimebadili sura ya Mtaa huo.
Huku
Ndiko Maji haya yanapo elekea yametokea katika makazi ya watu na
yanaelekea katika Makazi ya watu hasa kwenye mkusanyiko wa watu huku
Katika Maghorofa ya Jeshi ...........
Eneo
hili ni Moja ya Chemba ambayo Haijatengenezwa na hakuna mfuniko ipo
nyuma ya TRA Mwenge kuna majani haya lakini chini ni Chemba mtu akifanya
kosa hapa anazama . Lakini Mamlaka husika inalitambua hili na hakuna
anaye fanyia kazi hata kidogo
Hii
ni Chemba ya Pili ambayo nayo inatakiwa kupeleka Maji Baharini ni shimo
refu lakini hakuna usalama mfunuiko hakuna hakuna kitu chochote kile..
Miaka inapita Mamlaka husika hakuna anaye hangaika .
Hapa
ni eneo Sugu ambalo Lipo Jeshini pana Chemba ambayo ina muda mrefu
sana na hakuna anaye hangaika nayo ... Hapo Juu ya majani Pana hiyo
Chemba ya Maji Taka
Mtaa
Huo na eneo hilo hilo kuna Chemba ingine ambayo nayo imefumuka , kwa
mujibu wa wakazi wa eneo hili wanadai chemba hii ina Muda wa zaidi ya
Miaka 15
Mtaa
huu ambao umebatizwa jina la Kinyesi Street sasa hapo mbele ni Chemba
ingine ambayo ni tofauti na zote za awali nayo imefumuka kwa muda mrefu
na hakuna anaye hangaika kuja kufumua na kunyonya maji hayo machafu.
Bado
Eneo hilo hilo hii ni Chemba ingine kabisa ambayo nayo imefumuka na
kumwaga maji yake barabarani .. Wahusika bado wameulizwa wamesema hawana
Taarifa hii.
Uchafu
umezagaa eneo hili, Harufu mbaya imeendelea kutoka hapa.. hii ni Chemba
nyengine tena katika eneo moja ambayo nayo sasa imepasuka kutokana na
kuzidiwa na wahusika kuto lifanyia kazi swala hili...
Sasa
Maji Taka yote kutoka Mitaa yote sasa yanaingia katika Mfereji huu
mdogo ambao uliwekwa mahususi kama mvua zikinyesha basi maji yapite hapo
lakini sasa maji machafu toka chooni na matumizi ya binadamu ndio
yanapita hapa na mbaya zaidi yanapita katika makazi ya watu na
kusababisha harufu mbaya na kali.
Picha
Mbili za Juu Mtu unaweza ukazania kwamba ni mto unapita hapo tena
katika makazi ya watu, la hasha hayo ni maji ambayo ni Kinyesi kutoka
chooni.. Mkondo umekosa njia na kuamua kujipitia hapo.. Hali hii
imesababisha wananchi wapate shida sana kutokana na harufu mbaya inayo
waingilia majumbani mwao kila kukicha.. wamepiga kelele sana lakini
hakuna anaye sikiliza kilio chao.
Hapa
ni Mlangoni kwa mtu maji haya yanalazimisha Kupita lakini inashindikana
sasa yakijaa yanaingia moja kwa moja katika nyumba za watu hali ambayo
inaongeza kero zaidi
****
Wakazi wa mwenge mtaa wa umoja karibu kabisa na majengo ya
jeshi (JKT) wapo hatarini kupata magojwa ya mlipuko kutokana na mkondo
wakupitisha maji taka kujaa na kupasuka bila mamlaka husika kushughulikia na hivyo kuwa kero kubwa kwa wananchi wanaoishi
katika mazingira hayo.
Mmoja kati ya wananchi wanaoishi katika eneo hilo ambaye
hakutaka jina lake kuandikwa, kwa masikitiko makubwa amesema kuwa ni zaidi ya
mwezi sasa wamekuwa wakipata adhaa hii ya kujaa na kuziba kwa mikondo ya kupitisha
maji taka bila ya wahusika kuzibua
angali wanalipa tozo za kila mwezi
“Hali hii ya kujaa na kuzibuka kwa mikondo ya maji taka
imekuwa ikitokea mara kwa mara hasa kipindi cha masika na wakati mwingine wakati
wa kiangazi jambo lililopelekea hata mtaa huu kubadilishwa jina na kugeuzwa
kuwa ni mtaa wa kinyesi”
Wananchi hao wameituhumu mamlaka husika kwa kutokutambua majukumu
yao na hivyo kupelekea wananchi hao kuingia gharama mara kwa mara kwa kuamua
kuzibua wenyewe kwaajili ya kulinda afya zao.
Wananchi hao wanashindwa kuelewa kwanini mamlaka husika
inashindwa kutekeleza majukumu yake na kubaki kuchangisha pesa kwa wananchi
wakati mamlaka hizo zina mafungu ya fedha kwaajili ya marekebisho ya
miundombinu ya maji taka maarufu kama (service charge)
Pamoja na wananchi hao kufanya jitihada za kuwapata watu wa mamlaka
ya maji safi na maji taka DAWASCO lakini juhudi zao ziligonga mwamba baada ya
kuambia kuwa ni lazima wachangie fedha ya mafuta kwa sababu gari la mamlaka
hiyo halina mafuta.
Hofu kubwa ya wananchi wa maeneo hayo ni mvua, hasa katika
wakati huu unaoelekea kwenye kipindi cha mvua za masika ambazo zimekuwa na
madhara makubwa kwa upande wa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
---
---
Wakazi
wa eneo la mwenge kwa zaidi ya miaka mitano wamekuwa wakilishwa kinyesi
kinachotokana na kuzibuka kwa chemba za maji taka zaidi ya nane.
Chemba
hizo zimekuwa zikizibuka na kutiririsha maji machafu ya kinyesi na
kupita katika makazi ya wananchi wa maeneo hayo jambo ambalo ni hatari
kwa afya zao.
Pamoja
na jitihada za viongozi wa mitaa kutoa taarifa kwa wahusika hakuna
chochote kilichofanyika hadi leo jambo ambalo linatishia kuwepo kwa
magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu hasa wakati.
Mtdandao huu umekusanya matukio katika picha na video yakionyesha hali ilivyo...endelea kutazama chini ujionee mwenyewe...
0 comments:
Post a Comment