Mkurugenzi
wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Geita Gold Mine (GGM) Balozi Richard
Mariki (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyoya
kiserikali ya Benjamin William Mkapa Foundation (BMAF) Dkt. Ellen
Senkoro bahasha yenye nembo ya kampuni GGM kama ishara ya kupokea msaada
wa kiasi cha Sh. milioni 50 za kitanzania mbele ya waandishi wa habari
na baadhi ya watumishi wa BMAF.
Mkurugenzi
mtendaji wa Taasisi isiyoya kiserikali ya Benjamin William Mkapa
Foundation (BMAF) Dkt. Ellen Senkoro (kulia) akisisitiza jambo wakati wa
makabidhiano ya msaada wa kiasi cha Sh. milioni 50 za kitanzania mbele
ya waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa BMAF. Wa kwanza kushoto
ni Mkurugenzi wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Geita Gold Mine (GGM)
Balozi Richard Mariki.
Picha zote na Lorietha Lawrence-Maelezo
****
Taasisi
isiyoya kiserikali ya Benjamin William Mkapa Foundation (BMAF) imepokea
msaada wa kiasi cha Sh. milioni 50 za kitanzania kwa mwaka 2013 katika
kutekeleza mpango mkakati wake wa miaka mitano kwa awamu ya pili kati ya
mwaka 2012 hadi 2017.Makabidhiano hayo yalifanyika hivi
karibuni katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es
salaam kati ya Mkurugenzi mtendaji wa BMAF Dkt. Ellen Senkoro na
Mkurugenzi wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Geita Gold Mine (GGM)
inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu Balozi Richard
Mariki.
Dkt.
Senkoro alisema kuwa msaada huo kwa taasisis yake utatumika katika
mradi wa kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa upande wa ugonjwa wa
ukimwi (HIV/AIDS) na huduma kwa akinamama wajawazito na watoto wachanga
(MNH) kupitia mpango unaosimamia kuimarisha afya ya rasilimali watu
“Taasisi
yetu inaendelea na mpango wa kukusanya rasilimali kwa kuangalia malengo
ya muda mrefu kupitia marafiki na wahisani mbalimbali wakiwemo GGM na
makampuni mengine makubwa ndani na nje ya nchi.”alisema Dkt. Senkoro
Dkt.
Senkoro alisema kuwa BMAF katika kipindi hicho cha miaka mitano
inatarajia kukusanya jumla ya Sh. bilioni 12 za kitanzania ambapo lengo
ni kukusanya Sh. bilioni tatu za kitanzania kwa mwaka ili kuboresha
huduma za afya katika wilaya 15 nchini.
Dkt.
Senkoro alisema kuwa lengo ni kufikisha huduma kwenye wilaya 15 nchini
ambapo tayari wilaya sita zimeanza kunufaika na mradi huo ambazo ni
Kahama, Kishapu (mkoa wa Shinyanga), Sumbawanga vijijini, Kalambo na
Nkasi (mkoa wa Rukwa), na Biharamulo (mikoa ya Kagera).
Wilaya
nyingine zitakazonufaika na huduma hiyo kwa awamu ya pili zipo tisa
ambazo ni Shinyanga vijijini, Meatu, Bariadi, Halmashsuri ya mji wa
Sumbawanga,Maswa, Itilima, Busega, Mkoa wa kati-Pemba, na Chake- Unguja
vijijini.
Aidha,
Dkt. Senkoro alisema kuwa BMAF tayari imewaajiri watoa huduma 30 katika
maeneo ya watabibu, manesi na watoa huduma wasaididzi wa maabara ili
kufanikisha na kuboresha utoaji huduma na mradi huo kuwa endelevu.
Vivyo
hivyo Dkt. Senkoro alisema kuwa BMAF inawhudumu 32 tayari ambao wanatoa
huduma katika wilaya zilizoainishwa na itaendelea kuajiri wengine 30
katika Nyanja za kutoa huduma kwa wagonjwa wa ukimwi, huduma ya haraka
kwa akinamama wajawazito ambazo ndizo nyenzo mahususi kwa kuokoa maisha
ya akinamama hao wanapokuwa na matatizo wakati wa kujifungua.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Geita Gold Mine
(GGM) inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu Balozi
Richard Mariki alisema kuwa wanafarijika kuona msaada wanaotoa unatumika
kulingana na maelengo yaliyokusudiwa.
Vivyo,
Balozi Mariki ameishukuru BMAF kwa kuchagua kushirikiana na GGM katika
kutoa huduma kwa jamii na ameahidi kuendelea kushirikiana nao kwani wote
wanalenga kumhudumia mwananchi mhitaji.
Katika kutekeleza mpango mkakati wake wa awamu ya pili miongoni mwa wafadhili ambao BMAF inashirikiana nao ni NSSF, PPF, Shirika la Bima ya Afya la Taifa (NHIF),
LAPF, kampuni ya SWISSPORT, Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Banki Kuu ya
Tanzania, Banki ya NBC, NMB, CRDB, Stanbic, Serikali ya Ireland kupitia
mfuko wa Irish na Shirika la ndege la Precision.
0 comments:
Post a Comment