Rais
Uhuru Kenyatta akiwa kwenye mazungumzo na msanii Akon kwenye Ikulu yake
jijini Nairobi.(Picha zote kwa hisani ya ukurasa wa Facebook wa Rais
Uhuru Kenyatta).
Na Mwandishi wetu
Mwanamuziki
nyota wa R&B kutoka Marekani mwenye asili ya Senegal, Akon
amekutana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kufanya mazungumzo nae juu
ya mpango kusambaza umeme katika eneo la Kibera na sehemu nyingine za
vijijini zisizokuwa na nishati hiyo.
Mpango
huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wake wenye lengo la kugawa umeme
kwa mamilioni ya kaya katika bara la Afrika mpaka kufikia mwishoni mwa
mwaka.
”Napenda
kumpongeza Akon kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wa kiafrika na
napenda kuwatia moyo wengine kuiga mfano wake. Sisi tunaukaribisha
mpango huu na tutakuwa nae bega kwa bega” aliandika Rais Uhuru kwenye
ukurasa wake wa Facebook.
Rais Uhuru Kenyatta kwenye picha ya pamoja na Akon.
Rais Uhuru Kenyatta akimtembeza Akon kwenye baadhi ya maeneo ya Ikulu ya nchini Kenya mara baada ya mazungumzo.
CHANZO: HIKI HAPA
0 comments:
Post a Comment