Mshambuliaji wa Ngorongoro Heroes, Saad Kipanga, akiwania mpira na beki wa Nigeria, Omego Izuchukwu, wakati wa mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Afrika kwa timu za chini ya Umri wa miaka 20. Katika mchezo huo uliomalizika hivi punde Nigeria wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuondosha matumaini ya Ngorongoro kushinda katika mchezo wa marudiano unaotarajia kuchezwa Nigeria.
Mshambuliaji wa Ngorongoro, Iddi Seleman (kulia) akimtoka beki wa Nigeria, Ndidi Onyinye, wakati wa mchezo huo.