Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala akisisitiza umuhimu wa
mkutano wa wadau wa TEHAMA katika nchi za Bonde la Ufa na msatakabali wa vyombo
vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia kwenda dijiti
Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akifungua mkutano wa siku mbili wa
wadau wa Teknolojia ya habari na
mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es
salaam
Baadhi ya washiriki wa mkutano
wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani)
akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano
(TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Mngondo (kulia)
akiwa miongoni mwa washiriki wa mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya
habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la Ufa leo jijini
Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano
wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani)
akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano
(TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (katikati)
akisalimiana na baadhi ya washiriki mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau
Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la
ufa leo jijini Dar es salaam.Picha
zote na Eleuteri Mangi
---
Na Eleuteri Mangi
Serikali
imejenga mazingira mazuri kwa wawekezaji ili kuvutia makampuni mbalimbali
kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano nchini.
Kauli
hiyo imemtolewa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame
Mbarawa alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari
na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es
salaam.
“Nawasihi
wajasiriamali katika mambo ya TEHAMA ndani ya nchi washirikiane na wenzao wa
nje ya nchi ili waweze kujijengea uwezo wa kukuza uchumi wa nchi yetu” alisema
Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa aliwasihi washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania inawakaribisha
wawekezaji kuja kuwekeza katika TEHAMA ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata
huduma ya mawasiliano katika maeneo yote nchini hadi vijijini.
Aidha,
Prof. Mbarawa alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya TEHAMA ni pamoja na
ukosefu wa nishati ya umeme vijijini, kumudu gharama za uendeshaji, ukosefu wa
vifaa vya sekta hiyo na usalama wa taarifa mbalimbali katika mitandao.
Kwa
upande wake Waziri wa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa Bunge kutoka Burundi,
Tharcisse Nkezabahizi alisema kuwa TEHAMA ni moja ya Nyanja muhimu inayotumiwa
katika nchi yake ikiwemo elimu na huduma za afya ambapo ni muhimu kwa nchi za
bonde la ufa kutumia teknolojia hiyo ili kukuza uchumi wan chi husika.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala
alisema kuwa mkutano huo umekuja wakati mwafaka ambapo nchi nyingi zinatumia
fursa iliyopo ili vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia
kwenda dijiti.
Tanzania
mpaka sasa imekuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika kutekeleza hatua
ya kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda dijiti mbapo hadi kufikia mwishoni
mwa mwaka huu takribani mikoa yote itakuwa imezima mitambo ya analojia kwenda
dijiti.
Nchi zinazoshiriki katika mkutano huo ni Burundi, Rwanda, Somaliland, Zambia, Sudani Kusini ikiwemo Tanzania ambayo imekuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa mara ya pili mfululizo pamoja na wadau wengine katika sekta hiyo.