SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, February 23, 2014

Vita ya uenyekiti Bunge la Katiba kati ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta,

  Aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta,
 Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge
-----
Kadiri siku zinavyosogelea uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, ndivyo mpasuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unavyozidi, kutokana na kuwapo kwa makundi mawili yanayojipanga kusimamisha wagombea na ambayo yameanza kuendesha kampeni kuchafuana.
 
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa makundi hayo ni yale yanayomsaidia aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambao wametajwa kutaka kuwania nafasi hiyo.
Hata hivyo, wakati Chenge akiwa hayuko tayari kuthibitisha nia yake hiyo, Sitta hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo. Lakini habari zinasema vigogo hao wameshajipanga kwa ajili ya mbio hizo za uchaguzi na sasa wanatafuta watu wa kuwasaidia.
Kwa habari zaidi Bofya na Endelaaaaaa......

0 comments:

Post a Comment