SAFI KIJANA WANGU: Kocha wa Stoke City, Mark Hughes akimpongeza mchezaji wake Charlie Adam baada ya kuishushia kipigo Man Utd.
RVP: Robin van Persie (20) akishangilia na wenzake wa Man Utd baada ya kuifungia bao la kusawazisha dakika ya 47 ya mchezo.
MAJANGA: Kocha
wa Man Utd, David Moyes akiwa na machungu baada ya timu yake kupigwa
huku wachezaji wake Jonny Evans na Phil Jones wakiumia ambapo Jones
alikimbizwa hospitali.
TIMU ya Manchester United imeendelea kusuasua katika Ligi Kuu ya
England baada ya kupokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Stoke City leo
ikiwa ni mechi ya nane kupokea vipigo katika ligi hiyo.
Mabao yote ya Stoke yamefungwa na Charlie Adam katika dakika ya 38 na
52 wakati bao la Manchester United likifungwa na Robin van Persie
dakika ya 47. Kwa matokeo ya leo, Man Utd imebaki na pointi zake 40.
Katika mechi ya leo, wachezaji wawili wa Man Utd, Jonny Evans na Phil
Jones waliumia ambapo Jones alikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi
baada ya kugongana na Jon Walters wa Stoke.
0 comments:
Post a Comment