SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, November 23, 2013

MH. LOWASSA ACHANGIA MAENDELEO YA ELIMU KATA YA KIGAMBONI JIJINI DAR


 Umati wa Wakazi wa Mji wa Kigamboni,jijini Dar es Salaam wakiongoza Msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa wakati alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa Swala,Tuamoyo Kigamboni,jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya hafla hupi ya kukabidhi madawati kwa shule mbali mbali za Msingi katika kata hiyo ya Kigamboni.Hafla hiyo iliandaliwa na Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa wakinamama wajasiliamali wa Kikundi cha Vikoba Kata ya Kigamboni.Kushoto ni Mwenyeji wake ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa.Mh. Lowassa ameahidi kukisaidia kikundi hicho sh. Mil 10 kwa ajili ya maendeleo ya kikundi hicho.



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wakazi wa Kata ya Kigamboni kwa kuwapungia mkono,wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Swala,Tuamoyo Kigamboni,jijini Dar es Salaam.


Mh. Lowassa na Mwenyeji wake Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa wakiangalia burudani mbali mbali zilizokuwa zikitolewa Uwanjani hapo.



Burudani mbali mbali.


Mh. Lowassa akipena mikono na Kinamama wa Kigamboni.


Diwani wa Kata ya Vijibweni,Mh. Suleiman Mathew nae alipata wasaa wa kutoa neno lake mbele ya mgeni rasmi.


Mratibu wa Elimu Kata ya Kigamboni na Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi,Raha leo,Mwl. Asha Ferouz akisoma lisala mbele ya mgeni rasmi.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea lisala ya Maendeleo ya Elimu kata ya Kigamboni kutoka kwa Mratibu wa Elimu Kata ya Kigamboni na Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi,Raha leo,Mwl. Asha Ferouz.



Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa akizungumza na Wananchi wake wa Kigamboni waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Swala,Tuamoyo Kigamboni,jijini Dar es Salaam leo.


Kinamama wa Kigamboni.


Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa (katikati mwenye kipaza sauti) akiwatambulisha baadhi ya watendaji wake.


Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa akizungumza na Wananchi wake wa Kigamboni waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Swala,Tuamoyo Kigamboni,jijini Dar es Salaam leo.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akiwahutubia wakazi wa Kigamboni.


wakielekea kukata utepe.



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule mbali mbali za msingi katika Kata ya Kigamboni jijini Dar es Salaam,wakati wa kuwakabidhi madawati 100,yaliyotolewa na Diwani wa Kata hiyo,Mh. Dotto Msawa.Wakati huo huo pia Mh. Lowassa ameahidi kuwaongezea wanafunzi hao idadi ya madawati mengine 100.


Baadhi ya wanafunzi wa shule mbali mbali za msingi katika Kata ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wakiwa wameketi kwenye madawati hayo mara baada ya kukabidhiwa.


Mh. Lowassa akiagana na wana Kigamboni.
NA ANKAL MICHUZI

0 comments:

Post a Comment