SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, November 23, 2013

Kampuni ya Pan African Energy inayoendelea na Ukarabati wa visima vya gesi imefanikiwa kukamilisha takriban asilimia 85 ya matengenezo katika visima vya gesi vya songosongo.


 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba akitoa ufafanuzi jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)jana jijini Dar es Salaam, juu ya kupungua kwa mgao wa umeme kutokana na kufanikisha ukarabati wa visima vya gesi kwa zaidi ya asilimia themanini na tano , kulia ni Meneja Uhusiano wa shirika hilo bi. Badra Masoud.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba (hayupo pichani) mapema hii jana jijini Dar es Salaam wakati  akielezea juu ya kupungua kwa mgao wa umeme kutokana na kufanikisha ukarabati wa visima vya gesi kwa zaidi ya asilimia themanini na tano.Picha zote na Eliphace Marwa


----- 
Na Hassan Silayo
 Kampuni ya Pan African Energy inayoendelea na Ukarabati wa visima vya gesi imefanikiwa kukamilisha takriban asilimia 85 ya matengenezo katika visima vya gesi vya songosongo.
 
 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mhandisi  Felchesmi Mramba wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari  jana jijini Dar es salaam.
 
 Mhandisi Mramba alisema kuwa matengenezo hayo ambayo yanategemewa kukamilika November 26 mwaka huu yameonesha mafanikio ikiwa ni pamoja na kuwa na kasi ya kuridhisha kuliko ilivyotegemewa kwa kipindi cha mda mfupi tangu matengenezo hayo yaanze.
 
 “kwa kweli napenda kuwaambia watanzania kuwa wenzetu wa Pan African wanaoendelea na ukarabati katika visima vya songosongo wamekuwa na kasi ya kuridhisha ambapo mpaka sasa wamekamilisha kiasi asilimia 85 ya matengenezo na tunatarajia mapaka kufikia leo jioni tutaweza kuleta asilimia 80 ya gesi na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la umeme hasa katika kipindi hiki cha ukarabati wa visima hivyo.
 
 Aidha Mhandisi Mramba alifafanua kuwa matengenezo hayo ambayo yalienda sambamba na kuzima mitambo kwenye visima hivyo yanafanyika kila mwaka ili kuboresha uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi.
 
 Akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua kuhusu vigezo va ugawaji wa umeme hasa katika kipindi hiki cha matengenezo Mhandisi alisema kuwa maeneo muhimu kama kwenye mahospitali na sehemu za usalama yanapewa kipaumbele kutokana na umuhimu wake katika jamii.

0 comments:

Post a Comment