SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, July 7, 2012

Walanguzi wa vyakula Ramadhani watakiona

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/pinda(3).jpg 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
Na Sharon Sauwa
Serikali imesema itachukua hatua stahiki inazoona inafaa wafanyabiashara watakaopandisha bei za vyakula wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ili kuwaepushia waumini wa dini ya Kiislamu mikwaruzo mikubwa.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akijibu swali la Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo bungeni mjini Dodoma jana.
Katika swali lake, Mbunge huyo alisema hivi karibuni waumini wa Kislaamu wataingia katika Mfungo wa Ramadhani na kwamba uzoefu unaonyesha kuwa wakati huo kunakuwa na mfumko mkubwa wa bei hususan katika vyakula.
Alihoji Serikali imejipangaje katika kuwasaidia Watanzania hao kwa kupambana na wafanyabiashara wanaopandisha bei ya vitu wakati huo.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema ni vyema wafanyabiashara kutotumia mwanya huo katika kupata utajiri kwa njia ambazo si halali.
“Tusipandishe bei za vyakula bila sababu za msingi, wote tutambue kwamba tunayo dhamana ya kuhakikisha kuwa hatutumii mwanya huo kujinufaisha wakati hakuna sababu ya kufanya hivyo,” alisema.
Hata hivyo, alisema kwa upande wa serikali watachukua hatua stahiki watakaziona zinafaa, ili kuhakikisha mwezi huo unapita bila mikwaruzo mikubwa.
CHANZO: NIPASHE 

0 comments:

Post a Comment