Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Stephen Masele akizungumza na wakazi wa mjini mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara baada ya kufanya ziara ya siku mbili ya kutembelea machimbo ya madini ya Tanzanite.Picha na Ashura Mohamed
****
Na Ashura Mohamed-Simanjiro
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini,Stephen Masele ameiamuru kampuni ya TanzaniteOne kuacha kumwaga maji kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Akizungumza jana na uongozi wa kampuni hiyo,Masele ambaye ni Naibu Waziri anayeshughulikia madini aligeuka na kuwa mkali mithili ya mbogo wakati akizungumzia suala hilo kwa viongozi wa kampuni hiyo.
Naibu waziri alitoa amri hiyo baada ya kuelezwa na wachimbaji wadogo alipofanya ziara ya kutembelea migodi yao kuwa kampuni hiyo inawamwagia maji mgodini na alipotoa amri hiyo gari lake lilisukumwa na wachimbaji hao.
“Sawa ninyi ni wawekezaji lakini Serikali haipo tayari kuona wachimbaji wadogo wananyanyaswa katika nchi yao hivyo niwaamuru kusitisha mara moja kumwaga maji hayo kwenye migodi ya wachimbaji wadogo,” alisema Masele.
0 comments:
Post a Comment