Mwili wa aliyekuwa muasisi wa Chama cha Siasa cha CHADEMA Bob Makani aliyefariki kwa ugonjwa wa moyo, unaagwa leo jijini Dar es Salaam katika viwanja Karimjee.
Mwili wa mwana siasa huyo mkongwe nchini aliyefariki akiwa na umri wa miaka 74 unatarajiwa kusafirishwa kuelekea mkoani Shinya katika wilaya ya Kishapu kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho kutwa.
Kutokana na msibahuo mzito Chama cha CHADEMA kimesema kitapeperusha bendera nusu mlingoti kwa muda wa siku saba.