SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 11, 2012

KUFANYA VURUGU, SIO WAISLAMU WA KWELI.


Rais mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi,akishuka kwenye gari lake.

Baadhi ya waumini wa kiislamu waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa msikiti wa Masjidl Muhajirina.

Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa msikiti wa Masjidl Muhajirina, akiwa pamoja na baadhi wa viongozi wa dhehebu la kislamu mjini Singida.Wa tatu kulia,ni Sheikh wa msikiti wa Masjidl Muhajirina,Sheikh Issa Nasoro Issa.

Sheikh wa manispaa ya Singida,Sheikh Issa Simba,akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa msikiti wa Masjidl Muhajirina wa Majengo.

Rais mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akitoa nasaha zake muda mfupi kabla hajazindua msikiti wa Masjidl Muhajirina wa Majengo, Singida.

Raisi mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi,(wa nne kutoka kushoto) akielekea kuzindua msikiti wa Masjidl Muhajirina

Rais mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi,akizinduka msikiti wa Masjidl Muhajirina mjini Singida.  Picha zote na Nathaniel Limu
RAIS mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Alhaj Ally Hassan Mwinyi, amesema kuwa vikundi vilivyozuka hivi sasa vinavyodai,pamoja na mambo mengine,vinaamsha waislamu waliolala ki- imani, sio waislamu wa kweli. 
Amedai watu   walioko kwenye vikundi hivyo ambao wengi ni vijana,wanafanya mambo ambayo hayakubaliki mbele ya Mwenyezi Mungu na jamii kwa ujumla,kwa kusingizia kuwa vitendo vyao, vinaimarisha dini ya kiislamu.
Mzee Mwinyi ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa msikiti wa Masjidl Muhajirina, uliopo mtaa  wa Majengo ,mjini Singida.
Alisema makundi hayo wanarubuniwa ili kufanya mambo maovu ikiwemo mauaji ya watu wasiokuwa na hatia yoyote,na kisha kusingizia dini ya kiislamu.
Alisema dini ya kiislamu misingi yake ni pamoja na kuzingatia amani,utulivu,uadilifu, unyenyekevu na uchaji wa kweli kwa mwenyezi Mungu.
“Lakini vikundi hivi kwa mfano cha Boko haramu cha Nigeria,kinachochoma moto makanisa na mali za viongozi wa madhehebu ya kikiristo na waumini wake,pia hujilipua kwa mabomu ndani ya makanisa huku waumini wakiwa kwenye sala.Al-shabab cha Somalia,wao wamejikita kwenye kuteka meli na kisha kushinikiza wapewa mamilioni ya fedha,ndio waachie meli,kweli dini ya kiislamu ndivyo inavyoagiza”,alihoji mzee Mwinyi.
Akifafanua zaidi,Mwinyi alisema kikundi kilichozuka hivi karibuni cha Mwamsho cha Unguja ambacho kinadai kimeanzishwa kwa lengo la kuamsha waumini wa kiislamu waliolala kiimani au kidini,kama ni kweli,vitendo vyake vinakizana na lengo lililokusudiwa.
Mzee Mwinyi alisema mwaka 1832 viongozi wa dini ya dhehebu la dini ya kikiristo waliomba eneo la ardhi kwa sultani Sayid Sayid,ili waweze kujenga kanisa,sulitani huyo bila kiyongo,aliwapa eneo la ardhi kubwa na walipomaliza kujenga kanisa,mtawala huyo alitoa msaada wa saa kubwa ambayo iliwekwa kwenye mnara wa kanisa.
“Toka wakati huo hadi sasa tawala nyingi zimepita na zote zimekuwa zikibariki harakati za waumini wa kikiristo za kukuza ustawi wa dini  yao.Sasa leo hii vijana wanataka kujionyesha kuwa wao ndio waislamu watu wengine wanaotaka amani,utulivu,kuheshimiana na kuvumiliana,sio waislamu”,alihoji.
Mzee Mwinyi amewataka wanavikundi hao kuwa kila wafanyalo,wamwone Mwenyezi Mungu mbelel yao.Wakikataa ukweli huo, wajue kuwa Mungu anawaona na anaona kila ovu walifanyalo.
Akifafanua, alisema Mwenyezi Mungu hawezi akatuma watu/kikundi kuchoma makanisa na mali za wakiristo,kuua watu kwa kujitoa mhanga.Matendo hayo ni ya kishetani tu,hayakubaliki kabisa.
Wakati huo huo,amewaagiza waislamu kutumia kikamilifu misikiti kwa ajili ya mambo yote ya kheri na pia  kumwabudu Mwenyezi Mungu.Kamwe misikiti isitumike kuleta migogoro,fitina,uhasama na misuguano ya aina yo yote.

0 comments:

Post a Comment