Saturday, December 31, 2011
I WISH YOU A HAPPY NEW YEAR!!
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, December 31, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
I WISH YOU A HAPPY NEW YEAR
Rais Kikwete Amwapisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha rasmi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, aliyemaliza muda wake. Hafla hiyo ya kumuapisha Balozi Sefue, imefanyika leo Ikulu Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phllemon Luhanjo, akisimamia zoezi hilo.
Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu wakuu, baada ya hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, December 31, 2011
2
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
TTCL nao wawapa pole waathirika wa mafuriko
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Bw. Said Amir Said (katikati) na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Amin Mbaga (kulia) wakimkabidhi sehemu ya msaada walioutoa kwa Mratibu wa Maafa Manispaa ya Ilala Bw. Mwasabite Elioth kwa ajili ya watu waliokubwa na mafuriko.
Baadhi ya Maofisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL wakiwa katika piocha ya pamoja na watoto yatima baada ya kuwapa vyakula mbalimbali kwa msimu huu wa sikukuuu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Bw. Said Amir Said (katikati) na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Amin Mbaga (kulia) wakimkabidhi sehemu ya msaada walioutoa kwa Mratibu wa Maafa Manispaa ya Ilala Bw. Mwasabite Elioth kwa ajili ya watu waliokubwa na mafuriko.
(picha na TTCL)
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, December 31, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Polisi wanawake Morogoro wasaidia kambi ya Wazee

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina chialo akimkabidhi zawadi za Mwaka mpya Bi. Haruna Selemani (54) anaeishi katika kambi ya wazee wasio Jiweza ya Fungafunga mjini Morogoro juzi. Zawadi hizo zimetoklewa na Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPFNET) mkoa wa Morogoro.Misaada hiyo yote ilikuwa na thamini ya Shilingi 300,000/=.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo akimkabidhi sehemu ya msaada kwa mtoto, Rose Juma (12) hapa Chialo akimkabidhi, Seleman Kisengo (12) ambapo watoto hao ni miongoni mwa watoto wanaoishi katika kambi hiyo ya wazee wasiojiweza ya Fungafunga.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, December 31, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Mbunge wa Kigamboni(CCM)Dk Faustine Ndugulile Atoa Tamko Kupinga Nauri Mpya Za Pantoni
Mhe. Dk Faustine Ndugulile Mbunge Jimbo la Kigamboni-CCM
=========
BUNGE LA TANZANIA
OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA KIGAMBONI
Kumb na: KIG/KVK/VOL.1/4 29 Disemba 2011
Mhe. Dkt John P. Magufuli (MB)
Waziri Wizara ya Ujenzi
Dar es Salaam
YAH: KUSUDIO LA ONGEZEKO LA VIWANGO VYA NAULI KATIKA KIVUKO CHA KIVUKONI-KIGAMBONI
Kichwa cha habari hapo juu chahusika.
Wananchi wa Jimbo la Kigamboni wamepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kusudio la kuongeza nauli za abiria, magari na vyombo vingine vinavyotumia huduma ya kivuko kati ya Kigamboni na Kivukoni kuanzia tarehe 1 Januari 2012.
Kivuko hiki ni kiungo muhimu kwa wananchi wanaoishi upande wa Kigamboni ambao wengi wao ni watu wa kipato duni na hawana ajira za kudumu. Ongezeko la nauli kwa asilimia 100 ni kubwa sana na litawaathiri kiuchumi. Nimepigiwa simu nyingi na kuletewa malalamiko mengi katika siku ya leo kuhusiana na mpango huu wa kuongeza nauli. Wananchi wanataka kujua ni vigezo gani vilivyotumika kufikia nauli hizi mpya; vyombo gani vilivyopendekeza, kupitisha na kuidhinisha nauli hizi na wanataka kujua kwa nini hawakushirikishwa katika mjadala wa nauli mpya.
Pamoja na ongezeko kubwa la wakazi na magari yanayotumia huduma ya kivuko, cha kushangaza ni kwamba mapato kwa siku yamekuwa ni takribani Tsh 8 milioni kwa siku kwa muda mrefu sasa.
Ni dhahiri kumekuwa na upotevu mkubwa mikononi kwa watumishi wasio waaminifu wa kivuko. Mapato mengi yanapotea kwa njia zifuatazo:
1. Baadhi ya watumishi wa kivuko kukatisha risiti hususan za magari kwa kutumia vitabu bandia.
2. Baadhi ya watumishi kuziuza tena tiketi zilizotumika badala ya kuzichana.
3. Baadhi ya watumishi na askari wanapitisha magari na abiria baada ya kupokea malipo ya pembeni.
Vilevile mafuta ya vivuko huuzwa kwa wavuvi wadogo wadogo katika maeneo ya Feri.
Mambo haya yote yanafanyika pasipo kificho, binafsi nimeshawahi kushuhudia yote niliyosema hapo juu yakifanyika na kuyatolea ripoti kwa uongozi wa kivuko.
Ninaamini kuwa hatua zifuatazo zikichukuliwa mapato ya kivuko hiki yanaweza kufika zaidi ya Tsh 13 milioni kwa siku:
4. Kudhibiti uuzaji wa tiketi za abiria na magari.
5. Kudhibiti ununuzi, utunzaji na matumizi ya mafuta yanayotumika kwenye vivuko.
6. Kudhibiti idadi ya watu na magari yanayovuka bila kulipia huduma hii.
7. Kupunguza gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya vibarua.
Kutokana na unyeti wa suala hili, nashauri zoezi hili lisitishwe ili kutoa fursa ya kujadiliana kuhusu upandishaji wa nauli na maboresho ya huduma hii kwa kushirikiana na wadau na wawakilishi wa wananchi katika Jimbo la Kigamboni.
Natumaini mapendekezo haya yatafanyiwa kazi ili kuepuka kuwabebesha mzigo wa gharama za uendeshaji wakazi wa Kigamboni wanaotumia huduma ya kivuko pale Feri.
Naambatanisha nakala ya barua yangu ya tarehe 19 Januari 2011 yenye kumbukumbu namba KIG/KVK/VOL.1/1 kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TEMESA ambayo ilitoa mapendekezo ya njia ya kuboresha huduma na vile vile kutaka ushirikishwaji wa wadau katika suala la ongezeko la nauli. Barua hii haijajibiwa hadi hivi sasa.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.
Wako katika ujenzi wa Taifa
Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (MB)
MBUNGE
Nakala:
1. Mhe. Mizengo Pinda (MB)-Waziri Mkuu
2. Mhe. Mecky Sadick-Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam
3. Waheshimiwa Madiwani wote-Jimbo la Kigamboni
4. Wenyeviti wa Serikali za Mitaa-Jimbo la Kigamboni
5. Mkurugenzi Mkuu-TEMESA
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, December 31, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
SALAM ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA
SALAM ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,
TAREHE 31 DESEMBA, 2011
Ndugu Wananchi;
Leo tunauaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012. Naungana nanyi Watanzania wenzangu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na bahati ya kuiona siku ya leo. Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao hawakujaaliwa kuwa nasi kwa kuwa wametutangulia mbele ya haki. Tuzidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema na sisi tuendelee kumuomba Mola wetu atujaalie rehema na neema tele katika mwaka ujao.
Friday, December 30, 2011
AIRTEL YAMWAGA MISAADA KWA WAATHIRIKA
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simuya Airtel ,Jackson Mmbando akizungumza kuhusiana na utoaji wa msaada uliotolewa na kampuni hiyo kwa kushirikiana pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-,pichani kati ni Meneja Masoko wa Airtel,Rahma Mwapachu.
Msaani wa filamu/muziki ajulikanae kwa jina kisanii Shilole akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 30, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Vodacom Yatoa Pole Vifo Vya Wanahabari Marehemu Halima Mchuka Na John Ngahyoma.
Dar es salaam Disemba 30, 2011. Kampuni ya simu ya mawasiliano ya Vodacom imepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za vifo vya wanahabari nguli nchini Bi. Halima Mchuka na Bw. John Ngahyoma.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, wanahabari hao wamefariki kwa siku tofauti akianza Halima juzi na baadae Ngahyoma aliyefariki asubuhi ya leo wote jijini Dar es salaam.
“Tunatoa mkono wa pole kwa familia za marehemu, waajiri wao na kipekee familia ya wanahabari nchini kwa kuondokewa na wapendwa wetu ambao walikuwa sehemu muhimu ya ujenzi wa tasnia ya habari na utangazaji nchini.”Alisema Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Mwamvita Makamba
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, wanahabari hao wamefariki kwa siku tofauti akianza Halima juzi na baadae Ngahyoma aliyefariki asubuhi ya leo wote jijini Dar es salaam.
“Tunatoa mkono wa pole kwa familia za marehemu, waajiri wao na kipekee familia ya wanahabari nchini kwa kuondokewa na wapendwa wetu ambao walikuwa sehemu muhimu ya ujenzi wa tasnia ya habari na utangazaji nchini.”Alisema Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Mwamvita Makamba
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 30, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
NMB MBEYA YATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MBEYA
Mkuu wa wilaya ya mbeya Evansi Balama akipokea msaada mafuta ya kupikia mahindi na maharage toka kwa meneja wa NMB tawi la mbalizi Bw.Nazareth Lebbi kwa niaba ya NMB makao makuu na kumwakilisha meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 30, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
JOHN NGAHYOMA WA BBC HATUNAYE TENA!!
John Ngahyoma(pichani), Mwandishi mkongwe wa habari Tanzania na Mtangazaji amefariki dunia hii leo asubuhi.
Kifo cha Ngahyoma aliyekuwa mtangazaji na mwandishi wa shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Tanzania akiripoti kutoka Dar es Salaam na viunga vyake kimekuja siku moja baada ya mtangazaji mwingine mkongwe wa kike aliyejizolea sifa kubwa ya utangazaji mpira Halima Mchuka kufariki ghafla huku mipango ya maziko yake ikiendelea.
Ngahyoma aliyewahi kufanya kazi katika vituo vya taifa vya redio cha Redio Tanzania Dar es Salaam na baade kujiunga na IPP Media katika vituo vya Redio One na ITV ambako pia aliondoka na kujiunga na BBC ameripotiwa kufariki hii leo jijini Dar es Salaam.
Tasnia ya habari nchini Tanzania kwa kipindi cha siku mbili itakuwa imeapatwa na pigo kubwa kufuatia vifo vya waanahabari hao wawili wa siku nyingi.
Marehenu Ngahyoma amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu na hata kwenda nchini India kwa matibabu zaidi kufuatia maradhi yaliyokuwa yakimsibu.
Taarifa ya haraka iliyotumwa katika mitandao ya kijamii (blogs) na Katibu Mkuu wa Jukwaa la wahariri (TEF) Neville Meena inasema msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea jijini Dar es Salaam jirani na kwa Mwandishi mwingine aliyefariki miezi kadhaa iliyopita Danny Mwakiteleko.
Aidha Meena ameomba mtu yeyote atakaekuwa na taarifa zaidi kuhusiana na mipango ya maazishi ya Marehemu Ngahyoma kumfikishia.
Blog hii inaungana na wanahabari wote Tanzania na duniani kutoa pole kwa familia ya marehemu akiwepo, mke, watoto, ndugu jamaa na marafiki wote kwa msiba huo mkubwa uliowafika wakati huu wa shamra shamra za mwaka mpya.
Mungu awatie nguvu na imani wote waliofikwa na Msiba huu.
Bwana Mungu alitoa na Bwana Mungu ametwaa Jina lake lihimidiwe.
Kifo cha Ngahyoma aliyekuwa mtangazaji na mwandishi wa shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Tanzania akiripoti kutoka Dar es Salaam na viunga vyake kimekuja siku moja baada ya mtangazaji mwingine mkongwe wa kike aliyejizolea sifa kubwa ya utangazaji mpira Halima Mchuka kufariki ghafla huku mipango ya maziko yake ikiendelea.
Ngahyoma aliyewahi kufanya kazi katika vituo vya taifa vya redio cha Redio Tanzania Dar es Salaam na baade kujiunga na IPP Media katika vituo vya Redio One na ITV ambako pia aliondoka na kujiunga na BBC ameripotiwa kufariki hii leo jijini Dar es Salaam.
Tasnia ya habari nchini Tanzania kwa kipindi cha siku mbili itakuwa imeapatwa na pigo kubwa kufuatia vifo vya waanahabari hao wawili wa siku nyingi.
Marehenu Ngahyoma amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu na hata kwenda nchini India kwa matibabu zaidi kufuatia maradhi yaliyokuwa yakimsibu.
Taarifa ya haraka iliyotumwa katika mitandao ya kijamii (blogs) na Katibu Mkuu wa Jukwaa la wahariri (TEF) Neville Meena inasema msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea jijini Dar es Salaam jirani na kwa Mwandishi mwingine aliyefariki miezi kadhaa iliyopita Danny Mwakiteleko.
Aidha Meena ameomba mtu yeyote atakaekuwa na taarifa zaidi kuhusiana na mipango ya maazishi ya Marehemu Ngahyoma kumfikishia.
Blog hii inaungana na wanahabari wote Tanzania na duniani kutoa pole kwa familia ya marehemu akiwepo, mke, watoto, ndugu jamaa na marafiki wote kwa msiba huo mkubwa uliowafika wakati huu wa shamra shamra za mwaka mpya.
Mungu awatie nguvu na imani wote waliofikwa na Msiba huu.
Bwana Mungu alitoa na Bwana Mungu ametwaa Jina lake lihimidiwe.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 30, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Afungua Msikiti wa Masjid AL Haramayn Donge Muwanda Wilaya ya Kaskazini B Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya kuufungua Msikiti wa Masjid AL Haramayn Donge Muwanda Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo,(kushoto) Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ali Juma Shamuhuna
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akikata utepe kama ishara ya kuufungua Msikiti wa Masjid AL Haramayn Donge Muwanda Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo,(kushoto) Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ali Juma Shamuhuna.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 30, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Rais Jakaya Kikwete Atoa Heshima za Mwisho Kwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)Marehemu Halima Mchuka
MTANGAZAJI wa muda mrefu wa iliyokuwa Redio Tanzania Dar esSalaam RTD na baadae Shirika la Utangazaji Tanzania (SHIUTA)Marehemu Halima Mchuka.
Thursday, December 29, 2011
Mwenyekiti Wa Jukwaa la Wahariri,Absalom Kibanda Ajiengua Kwenye Kamati ya Kutafuta Vazi la Taifa
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda
===========
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI
Itakumbukwa kwamba Desemba 15 mwaka huu, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi aliniteua kuwa mjumbe katika Kamati ya Kitaifa ya Kukamilisha Mchakato wa Kupata Vazi la Taifa.
Siku chache baada ya uteuzi huo, nilipokea wito wa kuitwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi kutokana na makala ambayo ilichapishwa katika gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 30 mwaka 2011.
Kufuatia mahojiano hayo, Desemba 21 nilifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako polisi na wanasheria wa serikali walinifungulia mashtaka ya kuwachochea askari kutoitii Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 29, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
DAR LIVE: DISNEYLAND YA BONGO MITAA YA MBAGALA JIJINI DAR!!
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 29, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
HALIMA MCHUKA KATUTOKA!!
Halima Mchuka (katikati) akizungumza jambo enzi za uhai wake . Kulia ni Eda Sanga aliyekuwa bosi wake
=======
MTANGAZAJI wa muda mrefu wa iliyokuwa Redio Tanzania Dar esSalaam RTD na baadae Shirika la Utangazaji Tanzania (SHIUTA) amefariki Dunia. Taarifa zilizopatikana hivi punde zinadai kuwa Mtangazaji huyo ambaye alikuwa na kipaji kikubwa cha utangazaji amefariki Usiku huu wa leo tarehe 29-12-2011 saa 9.00alfajiri kutokana na kupatwa na stroke ya gafla .
“Alikuwa na tatizo hilo jana mchana mara baada ya kutangaza kipindi cha salaam cha TBC-Taifa na akazidiwa ndipo alipopelekwa Hospitali na sasa ndiyo amefariki dunia.”alibainisha mmoja wa watangazaji wa TBC ambaye alikuwa jirani na mtangazji huyu. Halima Mchuka inaaminika kuwa alijiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam mwaka 1994 ambapo alifanya kazi katika idara ya Habari na idara ya mipango.
Wadau wengi wa RTD na baadae TBC-Taifa wanamkumbuka sana mama huyu wa watoto wawili kwa kuwa mwanamke wa awali kuangaza mpira katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na kati.
“Unapotaja mpira wa miguu wakai huu huwezi kusahau kipindi cha michezo cha RTD cha saa mbili kasorobo na huyu dada Halima Mchuka.”alibainisha Idd Pazi mmojawapo wachezaji nguli wa Tanzania wa wakati huo.
Kwa hakika si wasikilizaji wa RTD na wanamichezo tu bali ata watu wa Karibu ambao waliwahi kufanya nae kazi tunamtazama kuwa ni mtu mpole mwenye huruma na kusaidia wenzake pale penye tatizo ambalo yeye anaweza kulitatua.
”unajua huyu mama mimi ndiye aliyenisaidia kuweza kupata kazi kwenye taasisi hii nilikuwa wala simfahamu mtu ,amenisaidia sana.”kuficha ni dhambi alinidokeza mfanyakazi mmoja wa SHIUTA.
Mara ya mwisho kuongea na mwana mama huyu nilikuwa nikiwa Iringa alinipigia simu na kuniulizia taarifa za familia yangu na kuniambia nimtunze sana mtoto wangu lakini huku akiniambia na kutambua “ mbona leo unaongea kwa unyonge” ah “ Halima hapana ila nipo eneo ambalo watu wanasoma ndiyo maana naongea kwa sauti ya chini “nilimjibu wakati huo kwani nilikuwa makaba ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira- Iringa.
Mungu ailaze Roho ya BI Halima Mchuka pahala pema peponi Amina
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 29, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
HALIMA MCHUKA KATUTOKA
KAMPENI YA "Red Alert" INAYOENDESHWA NA VODACOM TANZANIA YAKUSANYA SHILINGI 6,284,000/= MPAKA SASA
Vodacom Tanzania inawashukuru wote ambao tayari wameshaonyesha upendo wao kupitia kampeni ya “Red Alert” na kufanikisha kukusanya shilingi 6,284,000/= kati ya December 22, 2011 hadi December 27, 2011.
Tunapenda kutoa wito wa kuendelea kuchangia Ndugu zetu waliopatwa na janga la mafuriko kwani bado wanahitaji misaada yetu,kwa Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja anaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS yenye neno MAAFA na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.
Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa
*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.
Hatua ya 2: Chagua 4 – Lipa Bili
Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni – weka namba 155990
Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu – weka namba yako ya simu
Hatua ya 5: Weka kiasi – ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea
Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri
Hatua ya 7: Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 29, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
000/= MPAKA SASA,
284,
KAMPENI YA "Red Alert" INAYOENDESHWA NA VODACOM TANZANIA YAKUSANYA SHILINGI 6
SUPER D NA MAFANIKIO KATIKA NGUMI!!
Aliyekuwa bondia wa ngumi za kulipwa Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye pia ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti na mkoa wa Ilala kimichezo amesema anajivunia mafanikio makubwa aliyoyapata katika mchezo wangumi katika kipindi cha mwaka 2011.
Akizungumza na waandishi wa habari Super D ambaye pia ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha alisema moja ya mafanikio ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi na kuwafikisha katika kiwango kizuri cha kuvuna matuna ya mchezo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Super D ambaye pia ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha alisema moja ya mafanikio ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi na kuwafikisha katika kiwango kizuri cha kuvuna matuna ya mchezo huo.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 29, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
TAARIFA YA KUFUKUZWA KWA WANAFUNZI WACHACHE VINARA WA UHALIFU KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Siku za hivi karibuni kumekuwepo taarifa na tahariri kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la kufukuzwa kwa wanafunzi wachache vinara wa uhalifu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Katika taarifa hizo kumekuwa na madai kwamba kabla ya uamuzi wa Baraza la Chuo wa kuwafukuza wanafunzi hao, milango ya mazungumzo na maridhiano kati ya uongozi na wanafunzi ilikuwa imefungwa, na kwamba wanafunzi hao hawakupewa fursa ya kusikilizwa na kujitetea mbele ya vyombo husika vya Chuo.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 29, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
TAARIFA YA KUFUKUZWA KWA WANAFUNZI WACHACHE VINARA WA UHALIFU KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
SARUJI YATUMIKA KUKARABATI BAADHI YA BARABARA YA LAMI - MBEYA
Ukarabati wa barabara wa aina yake tofauti na utaalamu yakinifu, mtandao huu umeshuhudia ukarabati ukiendelea eneo la Kanisa la Sabato barabara ya Mbalizi kutokea Meta jijini hapa ambapo Saruji imetumika kuziba viraka katika barabara hiyo, badala ya kutumia Lami ambapo huigharimu serikali kutokana na viraka hivyo kubanduka baada ya muda mfupi.
Hata hivyo viongozi wa kitaifa wamekuwa hawapitishwi katika barabara hiyo kwa hofu ya kugundua ubadhilifu huo kutokana na kila mwaka barabara hiyo kukarabatiwa na Halmashauri ya jiji kwa kutumia makandarasi tofauti tofauti.
CHANZO; BOFYA
Hata hivyo viongozi wa kitaifa wamekuwa hawapitishwi katika barabara hiyo kwa hofu ya kugundua ubadhilifu huo kutokana na kila mwaka barabara hiyo kukarabatiwa na Halmashauri ya jiji kwa kutumia makandarasi tofauti tofauti.
CHANZO; BOFYA
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 29, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
SAKATA LA WALIMU WA ST. FRANCIS MBEYA LACHUKUA SURA!!
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 29, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Tuesday, December 27, 2011
Arsenal 1-1 Wolves!!
Gunners frustrated as Hennessey produces a fine performance to nullify the hosts' attack after a header from Fletcher restored parity following Gervinho's opener
Arsenal were held to a 1-1 draw with Wolves as they failed to leapfrog Chelsea into fourth in the Premier League.
Arsenal were held to a 1-1 draw with Wolves as they failed to leapfrog Chelsea into fourth in the Premier League.
A goal from Gervinho gave the hosts the perfect start after 10 minutes, but the Gunners were pegged back by a Steven Fletcher header in the first half, and some fine saves from Wayne Hennessey throughout the game helped earn the Midland side a point, even after Nenad Milijas' sending off in the second half.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Tuesday, December 27, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
Arsenal 1-1 Wolves
Vodacom Tanzania Yagawa Msaada Wa Awamu ya Pili(Chakula)Kwa Waathirika wa Mafiriko Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule akimtiwsha Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mkunguni B, kata ya Hananasifu Bw. Andrew Mkude kiloba cha sukari. Vodacom ilikabidhi mchele, sukari, unga wa sembe, mikate na maji ya kunywa kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam wanaojihifadhi katika kambi ya Hananasifu juzi.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Tuesday, December 27, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Wananchi Walioathirika na Upanuzi Wa Uwanja Wa Ndege Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wananchi walioathirika na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar hapo katika ukumbi wa Chuo cha Karume Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.Kulia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi na kushoto yake ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundo Mbinu Mh. Issa Haji Ussi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifafanua lengo la Serikali la upanuzi wa uwanja wa kisasa wa ndege kwa nia ya kuongeza mapato ya taifa
Wakazi Wa Kota Za Gerezani Jijini Dar es Salaam Wagoma Kuhama
Mwanasheria wa wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani , Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) akizungumza na wateja wake. Dar es salaam jana kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Tuesday, December 27, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Wakazi wa Jangwani Dar es Salaam Walioathiriwa na Mafuriko Wakisafisha Vyombo Vyao Kwa Kutumia Maji Yasiyo Salama
Wakazi wa Jangwani Dar es Salaam walioathiriwa na mafuriko wakisafisha vyombo vyao kwa kutumia maji yasiyo salama pembezoni mwa makazi yao baada ya kurejea na kuendelea na maisha yao kama kawaida jana.
Picha na Fadhili Akida
Sunday, December 25, 2011
SALAAM ZA CHRISTMASS NA NEW YEAR TOKA KWA 24 SEVEN 365 BLOG
Kwa niaba ya Timu nzima ya 24 SEVEN 365 , Napenda kuchukua fursa hii kwanza kabisa kutoa Pole za dhati kwa ndugu zetu, jamaa na marafiki waliopatwa na maafa ya mafuriko Nyumbani Tanzania na wale wote waliopoteza maisha yao kutokana na maafa haya M/Mungu Azilaze Roho Zao Mahala Pema Peponi, Amin.
Tumepokea taarifa hizi za maafa kwa mshituko mkubwa mno na tumeguswa na hili M/Mungu awajaalie Subira na Ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu wote walio hospitali wakipatiwa matibabu awajaalie afueni wapone na wale ambao wapo kwenye kambi za Muda.
Pili napenda kukutakieni kila la kheri katika wakati huu wa kusheherekea sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya ni vyema tukatumia sikukuu hizi kuwa karibu na Familia, Ndugu , Jamaa, Marafiki na Kuwafariji Wagonjwa, Yatima, Masikini, Wenye shida mbalimbali kwa kujumuika pamoja nao kusherehekea siku hii kwa salama na amani, na pia kutafakari yale yote ambayo tumeyafanya katika kipindi cha chote cha mwaka mzima na nini tunatarajia kufanya mwaka ujao.
M/Mungu atujaalie afya njema, Maisha marefu, Atuondolee mambo mazito atufanyie wepesi, Atupe moyo wa kumkukmbuka Yeye na kumwabudu ipasavyo, Moyo wa Huruma kuwahurumia ndugu zetu, Moyo wa Upendo kuwapenda Ndugu zetu, Atuondoshee dhiki na umasikini, Matatizo na Shida Mbalimbali, Awabadilishe nyoyo zao viongozi wetu wanaojali maslahi yao binafsi awape mioyo ya kufanya kazi kwa maslahi ya Umma(Taifa kwa ujumla), Awape uzalendo wa kujali na kutumikia wananchi wao pasipo kujali DINI, RANGI, KABILA, n.k.
Na Mungu ajaalie Taifa letu liwe ni Taifa la Amani na Utulivu na ajalie pia Mataifa mengine Duniani ipatikane amani na kusiwepo machafuko yanayoendela hivi sasa, na atujaalie tufike mwaka mwingine na ayaongoze mambo yetu yaende vyema.
HAPPY CHRISTMASS & HAPPY NEW YEAR
MAY GOD BLESS YOU ALL, AMIN.
MAY GOD BLESS YOU ALL, AMIN.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Sunday, December 25, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Friday, December 23, 2011
MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AWATEMBELEA WANANCHI WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya wananchi waliohifadhiwa katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia majuzi, wakati Makamu alipofika katika Kambi hiyo leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha jijini kuanzia majuzi. Makamu alifanya ziara hiyo ya kutembelea baadhi ya kambi za waathirika leo Desemba 23.
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 23, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AWATEMBELEA WANANCHI WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM
KIJANA DOSSANTOS ‘BABA WA MAPACHA WATATU’ ATOA SHUKRANI KWA WALIOSAIDIA KUNUSURU MAISHA YA WANAE.
Mmoja wa Wasamaria Wema Dada Norah alipowatembelea Mapacha hao hivi Karibuni
Watoto mapacha katika pozi.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 23, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
KIJANA DOSSANTOS ‘BABA WA MAPACHA WATATU’ ATOA SHUKRANI KWA WALIOSAIDIA KUNUSURU MAISHA YA WANAE.
VODACOM TANZANI YATOA MSAADA KWA WAADHIRIKA WA MAFRKO JIJINI DARES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadiq Meck Sadick ksuhoto akiwa na Mbunge wa Kinondoni Bw. Iddi Azan akipokea magodoro kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule .Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Vodacom Bi. Najengwa Mbagga. Vodacom imekabidhi magodoro 430, mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 30 milioni kusaidia kambi za waathirika wa maafa ya
Dar es salaam.
Sehemu ya watoto wanaoishi katika kambi ya waathirika ya maafa ya Dar es salaam katika kambi ya shule ya msingi Mchikichini wakiwa na magodoro yaliyogawiwa na Vodacom kwa waathirika wanaoishi katika kambi hiyo. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 23, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Ziara Ya Rais Jakaya Kikwete Alipowatembelea Waathirika Wa Mafuriko Jijini Dar es Salaam
Raisi Kikwete akiongea na waathirika wa mafuriko waliopewa hifadhi katika shule ya msingi mchikichini jana
Raisi Kikwete akiendelea kuongea na Waathirika Wa Mafuriko
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 23, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
BEI YA MADAFU LEO!!
NA ANKAL MICHUZI.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 23, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
BEI YA MADAFU LEO
MADIWANI MBEYA WAMPA MEYA KAPUNGA SIKU SABA KUJIELEZA, JUU YA UBADHIRIFU NA UCHOCHEZI
Mstahiki wa jiji la mbeya Athanas Kapunga
******************
KIKAO CHA BARAZA KUU LA MADIWANI JIJI LA MBEYA KIMEMALIZIKA HUKU MEYA WA JIJI LA MBEYA ATHANAS KAPUNGA AKIZIDI KUWEKWA KIKAANGONI, AMBAPO MADIWANI WA BARAZA HILO WAMEMPA SIKU SABA KUJIELEZA JUU YA TUHUMA MBALIMBALI ZINAZOMKABILI IKIWEMO,
******************
KIKAO CHA BARAZA KUU LA MADIWANI JIJI LA MBEYA KIMEMALIZIKA HUKU MEYA WA JIJI LA MBEYA ATHANAS KAPUNGA AKIZIDI KUWEKWA KIKAANGONI, AMBAPO MADIWANI WA BARAZA HILO WAMEMPA SIKU SABA KUJIELEZA JUU YA TUHUMA MBALIMBALI ZINAZOMKABILI IKIWEMO,
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 23, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
MAFURIKO YA DSM YALETA UHABA WA MAFUTA YA MAGARI MBEYA
BP Mbeya mjini ndiyo kituo chenye mafuta jijini hali hii ya kukosekana kwa mafuta Imedaiwa na wamiliki wa vituo hivyo vya mafuta kuwa imesababishwa na mafuriko yanayoendelea jijini DSM hivyo kukwama kwa magari ya kubeba mafuta hayo na kuyaleta mikoani
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 23, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
LIBENEKE JIPYA LA MASUALA YA JAMII KWA UJUMLA TOSA MAWE!!
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, December 23, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Thursday, December 22, 2011
RAIS KIKWETE AOMBOLEZA VIFO VYA WANANCHI 13 WA DAR ES SALAAM WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA MAFURIKO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa
Said Meck Sadiq kuomboleza vifo vya watu 13 ambao wamepoteza maisha katika mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua ambazo zimekuwa zinanyesha tokea jana, Jumanne, Desemba 20, 2011.
Aidha, Rais Kikwete amempa pole Mkuu huyo wa Mkoa kutokana na uharibifu mkubwa wa nyumba, makazi na mali nyingine za wananchi uliosababishwa na mvua hizo ambazo pia zimesababisha uharibifu wa miundombinu.
Rais Kikwete pia ameuelekeza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusaidiana na taasisi na vyombo vyenye uzoefu wa maafa kushirikiana katika kuendelea kuokoa maisha ya watu, kusaidia waliozingirwa na mafuriko na
kuwahifadhi na kuwasaidia wale wote waliopoteza nyumba na makazi kutokana na mafuriko hayo.
Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Sadiq: “Nimepokea
kwa masikitiko habari za vifo vya wenzetu 13 ilivyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo sote tumeishuhudia katika Mkoa wa Dar
es Salaam tokea jana.
Amesema: “Nakutumia wewe rambirambi zangu kutokana na vifo hivyo, na kupitia kwako kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika balaa hili la mafuriko. Wajulishe kuwa msiba wao ni msiba wangu, naelewa machungu yao na niko nao katika hali ya sasa ya maombolezo. Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Napenda pia kupitia kwako kutoa pole zangu nyingi kwa wote walioumia ama kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao wakati huu wa mazingira magumu.
“Chini ya usimamizi wako, ningependa kuona uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vyenye ujuzi na uzoefu wa kupambana na majanga na dharura za namna hii, kuhakikisha kuwa tunaendelea kuokoa watu ambao badowamezingirwa na mafuriko, tunawapa matibabu wale walioumia katika mafurikohayo, na tunawahifadhi na kuwapa huduma za kibinadamu wote waliopoteza nyumba na makazi yao katika mafurikio hayo.”
IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
DESEMBA 21, 2011
DAR ES SALAAM
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 22, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
RAIS KIKWETE AOMBOLEZA VIFO VYA WANANCHI 13 WA DAR ES SALAAM WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA MAFURIKO









