SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, December 29, 2011

SUPER D NA MAFANIKIO KATIKA NGUMI!!

Aliyekuwa bondia wa ngumi za kulipwa Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye pia ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti na mkoa wa Ilala kimichezo amesema anajivunia mafanikio makubwa aliyoyapata katika mchezo wangumi katika kipindi cha mwaka 2011.

Akizungumza na waandishi wa habari Super D ambaye pia ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha alisema moja ya mafanikio ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi na kuwafikisha katika kiwango kizuri cha kuvuna matuna ya mchezo huo.


Alisema pamoja na hilo pia ameweza kushirikiana vema na wadau wa ngumi pamoja na mapromota mbalimbali wanaoandaa mapambano makubwa kwa kutoa mchango wake wa vifaa vya ngumi ili kufanikisha mapambano mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka huu.

Katika hatua nyingine Super D amekua akitoa mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria mbalimbali kwa njia ya DVD zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo namashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khanny, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.
Alisema mipango yake kwa mwaka 2012 ni kuhakikisha anaendelea kuwainua mabondia wengine chipkizi akiwemo bondia Shomari Mirundi na Ibrahimu Class ambao amewataja ni mabondia wazuri wanaohitaji kuendelezwa vipaji vyao.

Alisema bondia Ubwa Salum ambaye alimtwanga Mustapha Doto,kwa pointi 60-57 alishinda ambapo pambano hilo lilikuwa moja ya mapambano ya utangulizi ya pambano kubwa la Rashidi Matumla na Maneno Osward lililofanyika DEsemba 25 mwaka huu.

Na  Father Kidevu

0 comments:

Post a Comment