SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, December 25, 2011

SALAAM ZA CHRISTMASS NA NEW YEAR TOKA KWA 24 SEVEN 365 BLOG


Kwa niaba ya Timu nzima ya 24 SEVEN 365 , Napenda kuchukua fursa hii kwanza kabisa kutoa Pole 
za dhati kwa ndugu zetu, jamaa na marafiki waliopatwa na maafa ya mafuriko Nyumbani Tanzania na wale wote waliopoteza maisha yao kutokana na maafa haya M/Mungu Azilaze Roho Zao Mahala Pema Peponi, Amin.
 Tumepokea taarifa hizi za maafa kwa mshituko mkubwa mno na tumeguswa na hili  M/Mungu awajaalie Subira na Ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu wote walio hospitali wakipatiwa matibabu awajaalie afueni wapone na wale ambao wapo kwenye kambi za Muda.
Pili napenda kukutakieni  kila la kheri katika wakati huu wa kusheherekea sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya ni vyema tukatumia sikukuu hizi kuwa karibu na Familia, Ndugu , Jamaa, Marafiki na Kuwafariji Wagonjwa, Yatima, Masikini, Wenye shida mbalimbali kwa kujumuika pamoja nao kusherehekea siku hii kwa salama na amani, na pia kutafakari yale yote ambayo tumeyafanya katika kipindi cha chote cha mwaka mzima na nini tunatarajia kufanya mwaka ujao.
M/Mungu atujaalie afya njema, Maisha marefu, Atuondolee mambo mazito atufanyie wepesi, Atupe moyo wa kumkukmbuka Yeye na kumwabudu ipasavyo, Moyo wa Huruma kuwahurumia ndugu zetu, Moyo wa Upendo kuwapenda Ndugu zetu, Atuondoshee dhiki na umasikini, Matatizo na Shida Mbalimbali,  Awabadilishe nyoyo zao viongozi wetu wanaojali maslahi yao binafsi awape mioyo ya kufanya kazi kwa maslahi ya Umma(Taifa kwa ujumla), Awape uzalendo wa kujali na kutumikia wananchi wao pasipo kujali DINI, RANGI, KABILA, n.k. 
Na Mungu ajaalie Taifa letu liwe ni Taifa la Amani na Utulivu na ajalie pia Mataifa mengine Duniani ipatikane amani na kusiwepo machafuko yanayoendela hivi sasa, na atujaalie tufike mwaka mwingine na ayaongoze mambo yetu   yaende vyema.
HAPPY CHRISTMASS  & HAPPY NEW YEAR
MAY GOD BLESS YOU ALL, AMIN.

0 comments:

Post a Comment