SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, December 29, 2011

HALIMA MCHUKA KATUTOKA!!

Halima Mchuka (katikati) akizungumza jambo enzi za uhai wake . Kulia ni Eda Sanga aliyekuwa bosi wake
=======
MTANGAZAJI wa muda mrefu wa iliyokuwa Redio Tanzania Dar esSalaam RTD na baadae Shirika la Utangazaji Tanzania (SHIUTA) amefariki Dunia. Taarifa zilizopatikana hivi punde zinadai kuwa Mtangazaji huyo ambaye alikuwa na kipaji kikubwa cha utangazaji amefariki Usiku huu wa leo tarehe 29-12-2011 saa 9.00alfajiri kutokana na kupatwa na stroke ya gafla .
“Alikuwa na tatizo hilo jana mchana mara baada ya kutangaza kipindi cha salaam cha TBC-Taifa na akazidiwa ndipo alipopelekwa Hospitali na sasa ndiyo amefariki dunia.”alibainisha mmoja wa watangazaji wa TBC ambaye alikuwa jirani na mtangazji huyu. Halima Mchuka inaaminika kuwa alijiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam mwaka 1994 ambapo alifanya kazi katika idara ya Habari na idara ya mipango.
Wadau wengi wa RTD na baadae TBC-Taifa wanamkumbuka sana mama huyu wa watoto wawili kwa kuwa mwanamke wa awali kuangaza mpira katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na kati.
“Unapotaja mpira wa miguu wakai huu huwezi kusahau kipindi cha michezo cha RTD cha saa mbili kasorobo na huyu dada Halima Mchuka.”alibainisha Idd Pazi mmojawapo wachezaji nguli wa Tanzania wa wakati huo.
Kwa hakika si wasikilizaji wa RTD na wanamichezo tu bali ata watu wa Karibu ambao waliwahi kufanya nae kazi tunamtazama kuwa ni mtu mpole mwenye huruma na kusaidia wenzake pale penye tatizo ambalo yeye anaweza kulitatua.
”unajua huyu mama mimi ndiye aliyenisaidia kuweza kupata kazi kwenye taasisi hii nilikuwa wala simfahamu mtu ,amenisaidia sana.”kuficha ni dhambi alinidokeza mfanyakazi mmoja wa SHIUTA.
Mara ya mwisho kuongea na mwana mama huyu nilikuwa nikiwa Iringa alinipigia simu na kuniulizia taarifa za familia yangu na kuniambia nimtunze sana mtoto wangu lakini huku akiniambia na kutambua “ mbona leo unaongea kwa unyonge” ah “ Halima hapana ila nipo eneo ambalo watu wanasoma ndiyo maana naongea kwa sauti ya chini “nilimjibu wakati huo kwani nilikuwa makaba ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira- Iringa.
Mungu ailaze Roho ya BI Halima Mchuka pahala pema peponi Amina

0 comments:

Post a Comment