ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A LOWEST COST AND ALSO SEND TO US NEWS, EVENTS FOR MORE INFORMATION CONTACT US TELEPHONE: +919160901191 E-mail: ally.shaaban@yahoo.com | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU NA PIA TUTUMIE HABARI, MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +919160901191 Barua Pepe: ally.shaaban@yahoo.com | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI HAPA

Friday, December 31, 2010


new year 2011 greeting

 Diaby aumia tena Aboua
Kiungo wa Arsenal Abou Diaby huenda asiendelee kucheza soka kwa muda mwingine mrefu, baada ya kutengua msuli wa mguu, ikiwa ni muda mfupi baada ya kupona jeraha lake la awali la kiwiko cha mguu.
Arsenal yapata pigo la mchezaji
Mfaransa huyo, aliingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Chelsea walioshinda 3-1, baada ya kutocheza kwa wiki tisa.
Hata hivyo alitoka akichechemea katika sare ya 2-2 dhidi ya Wigan.
"Ni kutenguka kwa msuli," amesema meneja Arsene Wenger, akizungtumza na wavuti wa Arsenal. "Hatocheza kwa muda kidogo, wiki kadhaa nadhani."
Abou Diaby
Diaby alivunjika mguu, na kutengua kiwiko mwaka 2006, kabla ya kurejea tena uwanjani.
Tatizo la kuendelea kuumia kwa mchezaji huyo wa Ufaransa kutaleta wasiwasi katika kikosi cha Arsenal ambacho kinapigana na vigogo wengine katika nafasi za juu katika msimamo wa ligi kuu ya England.
Manchester United iko kileleni, ikiwa pointi sawa na mahasimu wao wa mji mmoja, Manchester City, tofauti ikiwa ni magoli huku zote zikiwa na pointi 38.
Diaby
Sare dhidi ya Wigan iliipokonya safasi Arsenal ya kuwa na pointi sawa na timu hizo za Manchester, na hivy kusalia katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36.
Tatizo la mwanzo kwa Diaby lilianza mwezi Septemba baada ya kufanyiwa rafu na mlinzi wa Bolton Paul Robinson.
Kiungo huyo wa Arsenal alikaa nje kwa wiki tisa kutokana na jeraha la kiwiko cha mguu baada ya kucheza dhidi ya Birmingham Oktoba 6, ambapo Arsenal ilishinda 2-1.
Diaby ameichezea Arsenal mara tisa tu msimu huu katika mechi za ligi kuu, na kufunga bao moja tu.
Diaby alitokea Auxerre ya Ufaransa mwaka 2006 kwenda Arsenal kwa thamani ya Pauni milioni 2.
PASAPASA 2011 NEW YEAR EVE

Thursday, December 30, 2010

School out! 10- year- old Wonderkid to stand Tall in University!!
Sushma Verma
The admission committee of the Lucknow University (LU) had lately been wracking its brains over an exceptional case - whether or not to induct a 10-year-old girl in its BSc course.
    After some serious deliberation, the panel concluded that since Sushma Verma had already cleared her matriculation and intermediate examinations, she was entitled to study graduation courses.
    Sushma's track record has been consistently stunning. She cleared class X with 59 per cent marks from the UP Board in 2007, when she was only seven. This year, she passed the intermediate exam with 62 per cent marks from St Miraj Inter College.
    Her admission to the LU was initially withheld because of her age. However, she moved an application before the committee, urging it to reconsider the decision because she didn't want to waste a year and miss the academic session of 2010. "There is no specific mention of the minimum age limit in the rule book of the university. So, Sushma can be given admission," the committee observed, responding to her plea.
    According to university spokesperson S.K. Dwivedi, the committee was of the unanimous opinion that such students should be encouraged."While deciding Sushma's case, we have reached the conclusion that such students who have cleared their intermediate this year with good marks should be admitted for graduation courses," Dwivedi said. "Their age shouldn't be a bar. In fact, it is a proud moment for us to have a 10-year-old undergraduate who is confident of excelling in life," he added.
    Sushma's achievement is all the more creditable because she comes from a family which has limited means. Her father Tej Bahadur is a daily wager at the school she completed her intermediate course from.
    Sushma's brother Shailendra Verma, too, is a child prodigy, having secured admission in LU's Bachelor of Computer Applications course in 2009, when he was only 14.
    He, however, opted for a career in website development. "My son is doing something extra- ordinary. Big companies have hired him to tweak their websites," Shailendra's homemaker mother Chhaya Verma said. "My daughter will take admission in the CMS Girl's Degree College, which is affiliated to the LU. She has opted for zoology, botany and chemistry," Bahadur. a class eight dropout, said. "At the same time, she is preparing for medical entrance tests. Sushma wants to become a doctor," he added.
    Not only is Sushma a budding talent, the wonder kid is grounded as well. "There is nothing extraordinary about us. It is just that my brother and I take our education seriously. This is because my father is a dropout and mother unlettered. My dream is to open a hospital to treat poor people free of cost," she said humbly.
    St Miraj's principal Anita Ratra was full of praise for her. " She is an excellent student with a special flair for graphics. She secured a first division in her Class XII exams," Ratra said.
Chidi Benz kuwa Mtangazaji!!
chidi_benz
Chidi Benz
Msanii maarufu kwa kufoka foka Rashid Makwilo aka Chidi Benz anatarajiwa kutokea kwenye Luninga kama mtangazaji wa Televisheni ya East Africa TV, Channel 5. Akichonga na Bongo5 Chidi Benz alisema kimya chake cha muda mrefu hakikuwa bure bali alikuwa anajaribu kuweka mambo yake sawa ili aweze kuingia mwaka 2011 kwa kishindo cha ajabu.
"Nimejipanga vya kutosha katika idara zote za tasnia ya burudani kuanzia kimuziki hadi mambo mengine".
Akiendelea chidi benz alisema kwamba sasa amejipanga kurudi kwenye fani ya muziki kama msanii wa kweli kwani ana mapini ya ukweli ambayo unaweza peleka na yakasikilizwa na kupendwa mahala popote ulimwenguni na si Tanzania ama Afrika pekee.
"Nimesharekodi nyimbo za kutosha, siku si nyingi utamsikia chidi ambaye hamtomdhania.
Akichonga kuhusiana na mchakato huo wa yeye kutangaza kwenye luninga Chidi alisema kipindi chake ambacho bado hakijapewa jina ambacho kinatarajiwa kuanza kuonekana siku za karibuni kitakuwa ni maisha ya ukweli ama uhalisia kwa kifupi (Reality Show) wa maisha yake akiwa katika mishe na game ya HipHop.
chanzo: bongo5.com
Arsenal yan'gan'ganiwa na Wigan 2-2
Arsenal imelazimishwa kwenda sare na Wigan ya magoli 2-2.
Wigan wakicheza nyumbani ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Arsenal kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Ben Watson katika dakika ya 18.
Watson
Ben Watson.
Arsenal walikuja juu ya kulisakama lango la Wigan na kuppata mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za 39 na 44, kupitia Andrey Arshavin na Niklas Bendtner.
Wakiwa wanaelekea kupata ushindi wa pili mfululizo baada ya kuizaba Chelsea, Arsenal walijikuta wakienda sare baada la mlinzi wa Arsenal Sebastian Squillaci kujifunga, zikiwa zimesalia dakika tisa mpira kumalizika.
Squilacci
Sebastian Squilacci alijifunga.
Kwingineko Chelsea ilizinduka na kupata ushindi wake wa kwanza baada ya michezo saba, kwa kuifunga Bolton bao 1-0.
Bao hilo pekee lilifungwa na Flourent Malouda katika dakika ya 61.
Malouda
Flourent Malouda.
Liverpool nayo ilishindwa kutamba nyumbani baada ya kuchapwa bao 1-0 na Wolves ambao wako mkiani.
Bao hilo pekee lilifungwa na Stephen Ward katika dakika ya 56.
Liverpool ilishindwa kuonesha cheche zake licha ya nahodha Steven Gerrard kurejea uwanjani.
Wolves wamepata ushindi huo kwenye uwanja wa Anfiled ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 26.
Ushindi wa Chelsea umeipeleka timu hiyo hadi na fasi ya nne, juu ya Tottenham. Arsenal imesalia katika nafasi ya tatu, huku Manchester City ikiwa nafasi ya pili na Manchester United katika nafasi ya kwanza, licha ya kuwa pointi sawa na City.

Wednesday, December 29, 2010

Gbagbo hababaishwi na Tishio!!
Bw Gbagbo
Viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wamemaliza ziara yao nchini Ivory Coast ya kumshawishi Laurent Gbagbo kuachia madaraka, kufuatia kumalizika kwa uchaguzi wa urais wenye utata.
Bw Gbagbo anagoma kuachia madaraka kwa Alassane Ouattara, ambaye anatambulika kimataifa kama rais aliyechaguliwa.
Ujumbe wa viongozi hao umesema iwapo ataendelea na msimamo wake, anaweza kutolewa kwa nguvu za kijeshi.
Hatarini
Televisheni ya Ivory Coast ambayo inamtii Bw Gbagbo imewashambulia wanaomlaani kiongozi huyo kwa uamuzi wake wa kusalia madarakani.
Imesema, wananchi wa mataifa mengine ya Afrika wanaofanya kazi nchini humo huenda wakawa hatarini iwapo vitisho vya nguvu ya kijeshi vitaendelea kutolewa.
Mapema, askari wa kulinda usalama wa Umoja wa Mataifa alijeruhiwa mkononi kwa kupigwa na panga, wakati msafara wake uliposhambuliwa na kundi la watu katika ngome ya Bw Gbagbo.
Kuondoka
Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema moja kati ya magariu matatu kwenye msafara huo, lilichomwa moto, katika eneo la magharibi mwa mji wa Abidjan.
UN, ambayo ina zaidi ya wanajeshi 9,500 nchini Ivory Coast, imetuhumiwa na Bw Gbagbo kwa kuingilia masuala ya Ivory Coast, na kutakiwa kuondoka nchini humo.
UN imekataa kutii amri hiyo na kutaka utawala ukabidhiwe kwa Bw Ouattara.
UN
Wanajeshi wa UN wakilinda hoteli anayoishi Bw Ouattara
Taarifa iliyotolewa na Rais wa Cape Verde Pedro Pires ambaye ni mmoja wa viongozi watatu wa mataifa wa Afrika Magharibi, imesema ziara yao imemalizika na watakwenda Nigeria kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi wa Afrika Magharibi, Ecowas, Goodluck Jonathan.
Marais wa mataifa matatu waliofanya ziara ni, Rais Pires, Bon Yayi wa Benin, na rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma. Waliwasili asubuhi mjini Abidjan katika kile kinachoonekana kama hatua ya mwisho ya kumtaka Bw Gbagbo kuachia ngazi kwa njia ya amani.
Baada ya mkutano, rais wa Benin Boni Yayi alisema kila kitu "kimekwenda vizuri". Lakini mshauri wa Laurent Gbagbo, Abdon Bayeto, baadaye aliiambia BBC kuwa "ujumbe ambao Bw Gbagbo amewaambia ni kuwa yeye amechaguliwa kidemokrasia, na anatambuliwa kikatiba".
Marais hao watatu pia walikwenda kumuona Bw Ouattara, katika hoteli anayoishi, akiwa na baraza lake la mawaziri, huku wakilindwa na wanajeshi 800 wa UN.
POLISI, CUF 'VITA' DAR ES SALAAM
         Wafuasi wa Chama Cha Wananchi (CUF), wakiandamana kudai Katiba Mpya jana jijini Dar es Salaam.
Ilikuwa kama filamu kwa wakazi wa Dar es Salaam jana wakati baadhi ya viongozi na wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), walipolizidi maarifa Jeshi la Polisi katika kuhakikisha wanafanikiwa kupeleka mapendekezo ya rasimu ya Katiba Mpya, huku risasi za moto zikitumika kujaribu kuwatawanya.
Awali juzi, Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, lilizuia kufanyika kwa maandamano hayo kwa madai ya kuwapo kwa mkanganyiko wa taarifa ya namna ya uwasilishaji wa rasimu hiyo iliyotumwa kwenda Jeshi la Polisi na Wizara ya Katiba na Sheria.
Kwa mujibu wa Kova, taarifa waliyoituma CUF kwenda Wizara hiyo, haikutaarifu kuwa wangepeleka mapendekezo hayo kwa njia ya maandamano huku iliyotumwa kwenda Polisi, ikisema kuwa wangepeleka kwa njia hiyo, jambo alilosema lilikuwa na tofauti ya maana.
Saa tatu asubuhi jana, wanachama wa CUF walianza kukusanyika katika Ofisi za Makao Makuu zilizopo Buguruni, Ilala, ili kuanza maandalizi ya maandamano hayo ambayo kimsingi yalikuwa kinyume cha sheria.
Wakiwa hapo, wanachama hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali na kutumbuizwa na muziki uliokuwa ukipigwa na magari mawili ya matangazo ya chama hicho huku wakizifuatisha, ukiwamo wa ‘kama noma na iwe noma sikubali leo narivenji mimi’ ulioimbwa na msanii wa kizazi kipya, Kaka Man.
Ilipofika saa nne, magari matano ya Polisi huku yakiwa na askari wa kutuliza ghasia, yalifika hapo na kuwataka wanachama hao kusitisha maandamo kama vile ilivyoagizwa; lakini agizo hilo lilipuuzwa na wanachama hao na kusisitiza kutimiza azma yao ya kuandamana hadi wizarani.
Ilipofika muda huo, maandamano hayo yalianza, lakini yakiwahusisha wanachama peke yao waliokuwa wakitembea kwa miguu na kubeba mabango mbalimbali huku viongozi wao, akiwamo Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Julius Mtatiro, wakikwepa kuungana na wanachama hao na kutumia magari mawili kuondoka eneo hilo na kwenda wizarani eneo la Barabara ya Sokoine karibu na Magogoni.
Aidha, maandamano hayo yaliyokuwa yakipita katika Barabara ya Uhuru, yalipofika Buguruni Malapa yalikutana na ulinzi mkali wa askari hao na ghafla umati huo ulitawanyika na kukimbilia mitaani baada kuliona gari maalumu la Polisi Namba PT 0886, lililokuwa limebeba maji ya kuwasha.
Baada ya kukimbilia huku na huko, baadhi ya wanachama hao walikutana na kuungana tena katika Mtaa wa Kilwa na kuendelea na maandamano hayo, hali iliyowafanya askari Polisi kufyatua risasi za moto zaidi ya saba hewani ili kuwatawanya.
Kutokana na hali hiyo, waandamanaji hao walikimbia kuelekea maeneo mbalimbali huku magari ya Polisi zaidi ya 10 yakikatiza katika mitaa hiyo ya Ilala kwa lengo la kuwatawanya wanachama hao ambapo pia ilifanikiwa kuwakamata wanachama wanne waliopelekwa katika Kituo cha Polisi cha Karume.
Akizungumza baada ya kukabidhi rasimu hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Oliver Mhaiki, Mtatiro alisema rasimu hiyo yenye sura 36, Ibara 130 na kurasa 88, aliyosema iliandaliwa kwa miaka minne, imezingatia mahitaji ya Watanzania wa sasa, hivyo ni wajibu wa Serikali kuipitia na kuifanyia kazi ipasavyo.
Alidai Watanzania wamechoshwa na Katiba yenye viraka inayowaongoza kwa sasa, hivyo rasimu iliyotolewa na CUF imezingatia mahitaji yote muhimu na kwamba ndiyo mkombozi kwa maisha ya Watanzania masikini.
Alidai chama hicho kinajiandaa kulidai Jeshi la Polisi Sh milioni 10 sambamba na kuandaa maandamano mengine kwa ajili ya jeshi hilo kwa kile alichodai kuwa limevuruga maandamano yao licha ya kulipatia taarifa tangu Desemba 21, mwaka huu kuwa litafanya maandamano hayo.
Akipokea rasimu hiyo, Katibu Mkuu Mhaiki alisema atayawasilisha mapendekezo hayo kwa Waziri wake, Celina Kombani, kama ambavyo chama hicho kilivyokusudia kufanya huku akiwaomba viongozi hao kuwa watulivu wakati taratibu zingine zikiendelea kufanywa na Serikali.
Kwa upande wake, Kova akizungumza jana juu ya tukio hilo, alisema Polisi hawana ugomvi na chama hicho wala hawakuwazuia kupeleka rasimu hiyo, isipokuwa walitaka wapeleke kwa njia ya kawaida na siyo maandamano kama walivyofanya jana.
Alisema Serikali ilishazungumza suala la Katiba Mpya kuwa linazungumzika na linafanyiwa kazi, kwa hiyo maandamano ya chama hicho cha upinzani hayakuwa na tija yoyote.
Alisema wametumia nguvu za wastani kuwatawanya wana CUF na watu tisa wanashikiliwa na jeshi hilo na hakuna aliyejeruhiwa katika maandamano hayo, na Polisi kupitia Idara yake ya Upelelezi inafuatilia suala hilo ili kuangalia hatua gani itachukua kutokana na kukiukwa kwa amri yao.
            CHANZO: HABARILEO, PICHA RICHARD MWAIKENDA NA ROBERT OKANDA.

CHENGE ATIWA HATIANI, APIGWA FAINI!

Mbunge wa Bariadi Mashariki na aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria, Mhe. Andrew Chenge, leo asubuhi ametiwa hatiani na Hakimu wa Mahakama ya Kinondoni kwa makosa manne ya barabarabi, yakiwemo ya mauaji ya wasichana wawili aliowagonga kwa gari alilokuwa akiendesha na kuwaua, Machi 27, 2009, jijini Dar es salaam. Chenge ametiwa hatiani kwa makosa manne ya Kusababisha vifo vya wasichana wawili, Kugonga Bajaji, Kuendesha gari kwa uzembe na kuendesha gari isiyokuwa na Bima. Makosa yote hayo amepigwa faini ya shilingi za Kitanzania laki saba! (700,000/=) na amelipa. 
gari la Chenge lilohusika katika ajali hiyo
 
Bajaji iliyogongwa na kuua abiria wawili waliokuwemo, ambapo dereva alipona na hakupatikana hadi leo.

Tuesday, December 28, 2010

TAMASHA DOGO LA ZIFF 31- Dec – 2010 NGOME KONGWE.
ZIFF LOGO
TAMASHA dogo la Zanzibar International Film Festival (ZIFF) ambalo limepewa jina la ZIFF Min ZIFF lipo tayari kufanyika baada ya kutangaza filamu zitakazoonyeshwa katika tamasha hilo, Mini-Festival itakayofanyika Ngome Kongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 31/12/2010 hadi 2/01/2011, itakua ni Tamasha dogo la siku 3 katika kutoa muamko kwa Tamasha kubwa la ZIFF lijalo (2-10 Julai, 2011).
Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania pekee yake (Swahili Films) ili kuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili litaonyesha filamu 8 za Kitanzania na filamu 2 bora kati ya hizo zitaenda kuoneshwa katika Tamasha kubwa la filamu Afrika – FESPACO huko Burkina Faso.
Filamu hizo ni Best Wife, Don’t Cry, Briefcase, Huba, Divorce, This is it, Nani, na Black Sunday, mbili kati ya filamu hizi ndiyo zitakazochaguliwa na kuingia kwenye maonyesho ya filamu makubwa Afrika – FESPACO nchini Burkina Faso.
Kama ilivyo ada ya Tamasha la Filamu la Nchi za Majahazi, kutakuwa pia na makundi ya muziki na wakati huu kundi zima la THT litafanya maonyesho kwa siku zote tatu, watakao kuwepo ni Mwasiti, Marlaw, Mataluma, Amin, Barnaba, Pipi, THT Dancers na wengineo. Kwa habari zaidi tembelea www.ziff.or.tz
Tamasha la ZIFF limekuwa na mafanikio makubwa kimataifa mwaka huu. Tarehe 3-5 Decemba ZIFF ilionyesha filamu zake huko Potsdam Ujerumani ambako mtengenezaji filamu Sajani Srivastava alionyesha filamu ya Tanzania “Nani” ambayo iliwafurahisha sana watazamaji.ZIFF pia ilionyesha filamu zake katika tamasha la Trinidad and Tobago na pia inatarajia kuonyesha filamu zake huko New york African Art Museum mwaka ujao.
Tayari matayarisho ya Tamasha la 14 yameanza na kwa sasa kuna uhakika wa kuwa na Workshop juu ya utengenezaji filamu itakayoendeshwa na Deustsche Welle ya ujerumani.
Kwa upande wa Muziki Clouds Entertainment wameingia mkataba na ZIFF kuendesha shughuli za muziki katika ZIFF.
Bashir atakubali matokeo ya Sudan Kusini
Rais wa Sudan Omar al Bashir amesema atakubali uamuzi wowote ambao Sudan Kusini itaufanya katika kura ya maoni ya uhuru wa eneo hilo mwezi wa Januari mwakani.
Rais Bashir wa Sudan
Rais Bashir amesema Sudan Kaskazini itatoa msaada wowote utakaohitajika kwa Kusini, kama wataaamua kujitenga au la.
Bashir alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Al-Jazira katikati mwa Sudan.
Alisema serikali ya Sudan itawasaidia watu wa Kusini kuijenga nchi yao, kwa vile inataka taifa hilo liweze kujiendesha bila matatizo.
Rais Bashir mapemwa mwezi wa Desemba alisema sehemu ya kaskazini mwa Sudan, ambapo kuna Waislamu wengi, itaimarisha sheria za Kiislamu ama sharia, baada ya kura ya maoni.
Arsenal yainyuka Chelsea 3-1
Alex Song - Arsenal v Chelsea: match report
Alex Song, midifirda Arsenal baada ya kufunga bao la kwanza.
Arsenal imejikita katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya England baada ya kuizaba Chelsea 3-1.
Fabregas aliandika bao la pili
Mabao kutoka kwa Alexander Song, Nahodha Cesc Fabregas na Theo Walcott ndio yalizamisha meli ya mabingwa hao watetezi.
Bao pekee la kufutia machozi kwa Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic.
Arsenal sasa wamefikisha pointi 35, katika nafasi ya pili, huku Chelsea wakiendelea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa wa pointi 31


Sunday, December 26, 2010

***HAPPY BIRTHDAY ***
 
NASSIB JUNIOR
LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MDAU WA BLOG HII   NASSIB JUNIOR (NASS JR) WA WA HYDERABAD INDIA.
BLOG HII INAUNGANA NA FAMILIA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KUKUTAKIA KILA LA HERI KATIKA SIKU YAKO HII YA KUZALIWA.
MOLA AKUPE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU,BUSARA NA HEKIMA  KATIKA MAISHA YAKO.
HAPPY BIRTHDAY TO YOU MAN.
HAPPY NEW YEAR MAN ENJOY YOUR DAY.
************

Saturday, December 25, 2010

Ecowas yaitisha Ivory Coast kijeshi
Umoja wa Kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi Ecowas, umemuambia rais anayetetea kiti chake nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo kuachia madaraka, au atarajie kukabiliwa kutolewa kwa "nguvu kisheria".
Gbagbo
Jeshi la UN likifanya doria mjini Abidjan
Taarifa hiyo imekuja mwishoni mwa mazungumzo ya dharura juu ya mzozo wa kisiasa uliozuka kufuatia kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi.
Umoja huo wenye nchi 15 wanachama, pamoja na mashirika mengine ya kimataifa yamemtambua mpinzani wa Bw Gbagbo, Alassane Ouattara kuwa mshindi wa urais.
Baraza la Katiba la Ivory Coast linasema Bw Gbagbo alichaguliwa, likisema kulikuwa na wizi wa kura katika ameneo kadhaa.
Ouattara
Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara
Uchaguzi huo ulikuwa na lengo la kuiunganisha nchi hiyo, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002, kuligawanya taifa hilo ambalo linazalisha kakao kwa wingi zaidi duniani.
Siku ya Alhamisi, matangazo ya kituo cha televisheni cha taifa,yaliacha kuonekana katika maeneo kadhaa nje ya Abidjan.
Lakini licha ya shinikizo hilo la kimataifa, Bw Gbagbo ameendelea kun'gan'gania madarakani, akisema uamuzi wa Benki kuu ya Afrika Magharibi kutoa akaunti ya beni ya nchi kwa Bw Ouattara ni kinyume cha sheria.
Msemaji wa Bw Gbagbo, Ahoua Don Mello akisoma taarifa kupitia televisheni amesema ilikuwa ni "kinyume cha sheria na nje ya kanuni za benki, na kutakuwa na madhara makubwa".

***HAPPY BIRTHDAY ***
 MWINYI BOKO
IZZO BIZNESS
LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MDAU WA BLOG HII   MWINYI BOKO  NA MSAANII WA HIP HOP IZZO BIZNESS WOTE WA DARESSALAAM  TANZANIA.
BLOG HII INAUNGANA NA FAMILIA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KUWATAKIA KILA LA HERI KATIKA SIKU YENU HII YA KUZALIWA.
MOLA AWAPE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU,BUSARA NA HEKIMA  KATIKA MAISHA YENU.
HAPPY BIRTHDAY TO YOU ALL.
HAPPY CHRISTMASS ENJOY YOUR DAY.
************

Friday, December 24, 2010

Makamu Wa Rais Akutana Na Waziri Wa Mawasiliano Na Uchukuzi Wa Zambia Leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal kulia, akisalimiana na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Zambia Profesa Geoffrey Ligwangwa wakati Waziri huyo alipokwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais Oysterbay Dar es salaam leo kwa ajili ya kumkabidhi Ujumbe Maalum wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwa Rais Ruphia Banda wa Zambia

Thursday, December 23, 2010

Zimbabwe imetakiwa kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa wa amani
Rais Mugabe
Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi nyinginezo zimeitaka serikali ya umoja wa kitaifa ya Zimbabwe kufanya mabadiliko muhimu ili kuhakikisha uchaguzi wa mwaka ujao unafanyika kwa itibari, haki na amani. Taarifa iliyotolewa na nchi hizo sambamba na kukiri kupatikana kwa kiasi fulani maendeleo ya kiuchumi na masuala mengineyo, lakini imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuheshimiwa haki za binadamu, utawala wa sheria pamoja na kuheshimiwa makubaliano yaliyofikiwa na pande husika za nchi hiyo. Nchi hizo aidha zimesema kwamba, zitazishauri nchi jirani na Zimbabwe hasa Afrika Kusini kushirikiana na serikali ya Harare ili kutayarisha mazingira ya kufanyika uchaguzi huru, wa haki na wa amani. Rais Mugabe anasisitiza kufanyika uchaguzi mkuu katikati mwa mwaka ujao wa 2011 suala ambalo limeafikiwa pia na chama cha MDC kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Watu 173 wauawa ivory Coast
Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Ivory Coast zimesababisha vifo vya watu 173, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, huku shinikizo la kimataifa likiendelea kumkaba Laurent Gbagbo ajiondoe madarakani.
Mwanajeshi
Mwanajeshi wa UN mjini Abidjan
Umoja wa Mataifa umesema unatazama njia za kuimarisha jeshi lake nchini Ivory Coast, katika maeneo ambayo majeshi ya Bw Gbagbo yakiwa katika hali ya mvutano mkubwa na wafuasi wa mpinzani wake, Alassane Ouattara.
Ouattara
Ouattara na Gbagbo
Umoja wa Mataifa pia umethibitisha kuwa mamluki wa Liberia wanasaidia majeshi ya Bw Gbagbo.
Umoja wa Mataifa na nchi nyingine kadhaa duniani zimemtambua Bw Ouattara kama rais mpya.
Tume ya haki za binaadam ya Umoja wa mataifa inakutana mjini Geneva kujadili janga hilo. Tume hiyo imesema watu 173 wameuawa wiki iliyopita na karibu 500 kukamatwa nchini Ivory Coast.
Ivory Coast
Ghasia Ivory Coast
Mwandishi wa BBC Thomas Fessy mjini Abidjan anasema kuna taarifa nyingi za msako wa usiku katika makazi ya watu wanaomtii Bw Ouattara, na majeshi ya Bw Gbagbo yanazuia waandishi kwenda katika maeneohayo na ni vigumu kuthibitisha mauaji hayo.
Wafuasi wa Bw Ouattara wametaka Mahakama ya Kimataifa kuwashitaki washirika wa Bw Gbagbo kwa uhalifu wowote ambao umefanywa.
Bw Ouattara na wafuasi wake wanaishi katika hoteli mjini Abidjan, huku wakilindwa na majeshi ya kulinda usalama ya Umoja wa Mataifa wapatao 800.

Wabunge Kenya waipinga ICC
Wabunge wa Kenya wamepiga kura kutaka nchi hiyo kujitoa katika makubaliano yaliyofikiwa kuunda Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ya The Hague (ICC).
Kenya ghasia
Ghasia baada ya uchaguzi 200
Hatua hiyo inakuja wiki moja tu baada ya mwendesha mashitaka wa ICC kutaja majina sita ya watu anaowatuhumu kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi.
Orodha ya majina hayo imejumuisha wanasiasa wa ngazi za juu na wafanyakazi wa serikali.
Mwendesha mashitaka wa ICC Moreno Ocampo
Wabunge hao hawana uwezo wa kuleta mabadiliko yoyote ya haraka katika nchi kujiondoa katika makubaliano ya ICC, lakini wamefikisha ujumbe kwa serikali kuanza mchakato wa kujiondoa.
Takriban watu 1,200 walikufa na zaidi ya watu laki tano kukimbia makazi yao katika ghasia hizo zilizotokana na uchaguzi uliofanyika Disemba mwaka 2007.
Ghasia hizo zilimalizika baada ya Rais Mwai Kibaki na mpinzani wake Raila Odinga kukubali kugawana madaraka, Bw Odinga akipata wadhiwa wa waziri Mkuu.
Kibaki
Mwai Kibaki na Raila Odinga
Katika makubaliano ya amani yaliyofikiwa, ilikubaliwa kuwa waliosababisha ghasia hizo watafikishwa mahakamani nchini Kenya, au katika Mahakama ya Kimataifa mjini Hague.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi anasema iwapo serikali itaungana na wabunge, itachukua muda usiopungua mwaka mmoja kwa Kenya kujiondoa rasmi kutoka ICC, lakini kesi ambazo tayari zimefunguliwa hazitasitishwa.
Kutajwa kwa majina sita ya washukiwa kulisababisha mtikisiko mkubwa katika siasa za Kenya, anasema mwandishi wa BBC.
Wabunge
Wabunge wa Kenya
Katika orodha hiyo, yupo Uhuru Kenyatta, ambaye ni naibu waziri mkuu na mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya, jomo Kenyatta.
Pia wapo wanasiasa wengine wa ngazi za juu ambao ni washirika wa rais wa waziri mkuu, na pia mkuu wa zamani wa polisi.
Mtazamo wa kikoloni
katika majadiliano yaliyodumu hadi usiku, wabunge hao walisema ICC ina mtazamo wa kikoloni, ni mahakama inayopinga uafrika na kusema Kenya inauza uhuru wake.
"Ni Waafrika peke yake ndio wanashitakiwa na ICC," gazeti la kila siku la Nation limekaririwa likimkariri waziri wa nishati Kiraitu Murungi.
"Hakuma Mmarekani au Mwingereza atashitakiwa katika mahakama ya ICC, tusiruhusu kurejea wenyewe katika ukoloni," amesema.
ICC haikutufuata sisi, sisi ndio tuliikaribisha
Martha Karua
Mbunge mmoja pekee, Martha Karua, waziri wa zamani wa sheria ndiye alikuwa na mtazamo tofauti.
"ICC haikutufuata sisi, sisi ndio tuliikaribisha," alisema Karua.
"Iwapo Wakenya wanajiuliza kuhusu kutoshitakiwa, hii ndio sura yake halisi."
Mara ya kwanza
Mwandishi wetu anasema baadhi ya wabunge wanaamini itachukua miaka mingi kwa mchakato wa kisheria katika mahakama ya ICC kuanza kufanya kazi.
Hii ndio sababu waliamua kwenda katika mahakama ya kimataifa, badala ya mahakama ya Kenya.
Mwandishi huyo anasema walishitushwa wakati mwendesha mashitaka wa ICC Louis Moreno Ocampo alipotaja majina ya washukiwa, kwa sababu kwa mara ya kwanza katika historia ya Kenya, ilianza kuonekana kuwa wanasiasa wakubwa wasioweza 'kuguswa' huenda wakashitakiwa.

BALOZI WA UTURUKI AMTEMBELEA SPIKA

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anna Makinda, akimkaribisha Balozi wa Uturiki nchini Tanzania Dk. Sander Gurbuz alipomtembelea ofisini leo jijini Dar es Salaam.

Wednesday, December 22, 2010

Glitter Graphics
Kwa niaba ya timu nzima ya 24SEVEN365 ,Napenda kuchukua nafasi hii kwanza kutoa shukrani za dhati kwa ushirikiano wenu mnaotupa katika kipindi chote hiki na naomba tuzidi kushirikiana kwa hili na lile maana bila nyie sisi hapa hatuwezi kuwepo.Pili napenda kukutakieni  kila la kheri katika wakati huu wa kusheherekea sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya ni vyema kutumia sikukuu hizi kuwa karibu na Familia,Ndugu ,Jamaa na Marafiki kwa kuwa pamoja kupongezana na kusherehekea kwa salama na amani, na pia kutafakari yale yote ambayo tumeyafanya katika kipindi cha mwaka mzima na nini tunatarajia kufanya mwaka ujao.Mungu atujaalie tuuone mwaka mwingine na mambo yetu ayaongoze yaende vyema.
HAPPY CHRISTMASS  HAPPY NEW YEAR
GOD BLESS YOU ALL, AMIN.

Monday, December 20, 2010

RAIS ZANZIBAR AAHIDI KUTEKELEZA AHADI ZA WAKATI WA KAMPENI
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
Wanawake wa rika zote visiwani Zanzibar wametakiwa kutokuwa na hofu na kuhakikishiwa kuwa ahadi zote zilizotolewa na rais wakati wa kampeni zinazowahusu wao zitatekelezwa bila ya waiswasi.
Akizungumza katika viwanja vya Kisonge rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amesisitiza kuwa ahadi zote zitatekelezwa, ikiwemo sera ya wanawake na kundaa mpango maalum ili kuhakikisha wanawake nao wanapata nafasi za juu za kuongoza.
Rais huyo wa Zanzibar pia aliahidi kuwa serikali itahakikisha inapambana na vitendo vilivyoshamiri vya udhalilishaji wanavyofanyiwa wanawake na watoto.
Aidha nao  viongozi wa Umoja wa Wanawake akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja huo Bi. Amina Nassor na Makamu Mwenyekiti Zanzibar Bi. Asha Bakari pamoja na kumpongeza rais huyo pia walitoa wito kwa wanawake visiwani humo kuanza kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
MSHINDI WA BONGO STAR SEARCH APATIKANA
Mshindi wa shindano la Bongo Star Search 2010 ni Mariam Mohamed(pichani).Hafla ya kumpata mshindi wa shindano hilo ilifanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam mwishoni mwa wiki.
Jaji Salama Jabir akitoa maoni kwa mshiriki. Salama amekuwa kivutio kikubwa sana katika mashindano hayo kutokana na maoni anayotoa kwa washiriki lakini mashabiki wanamchukulia kama ni mtu mwenye kukatisha tamaa na kujilopekea tu la hasha, hiyo ni fani yake na anajua anachokifanya.
Nimekwambia kaa chini mimi ndio boss wako-Chief Judge Madam Ritha Paulsen akimkaripia kwa kumkalisha Jaji Master J baada ya kuwa mkaidi katika fainali hizo.
Mshiriki Joseph Pyne ambaye alishika nafasi ya 3 katika fainali hizo aliteka ukumbi mzima kwa kushangiliwa na kutunzwa pesa nyingi jukwaani kila alipopanda na kufanya mashabiki wake kuacha midomo wazi kutokana na kuimbia nyimbo ambazo mashabiki wanazikubali na kuzipenda.
Pichani ni baadhi ya mashabiki wa Joseph Pyne wakihamaki kwa kutoamini alichokuwa akiimba mshiriki huyo. Hebu tazama picha hii kwa umakini kila shabiki anaonekana kuhamaki wenggine waliamua kusimama wakiona kwamba wakika chini hawatofaidi vizuri..!!!
Wewe kuchukua milioni 30 usiku wa leo! i will shoot my self- Salama. Hayo ni maoni ya Jaji Salama Jabir kwa Mshiriki Joseph Pyne kwa mtazamo wake kwamba asipate kichwa kuona ukumbi nzima ukipiga nderemo kwa ajili yake.
Vijana wa THT wakitoa burudani wakati wa mapumziko mafupi huku washiriki wa BSS 2010 wakisubiri kufanyiwa mchujo wa raundi ya pili katika fainali hizo.
Mwanamuziki Mwasiti Almasi akitoa burudani katika fainali hizo.
TOP 5 ya BSS 2010 wakisubiri kuchujwa kuingia raundi ya pili katika fainali hizo ambapo mshiriki Waiziri Salum (wa kwanza kulia) alienguliwa na kuaga mashindano hayo lakini hakuondoka mikono mitupu alipata kitita cha shilingi milioni 1 kutoka Bench Mark Production pamoja na Ofa ya kurekodi nyimbo moja katika studio za MJ RECORDS pamoja na cheti cha kushiriki mashindano hayo.
Mother House wa jumba la BSS 2010 naye alikuwepo akishuhudia watoto wake walibyokuwa wakitawala jukwaa katika fainali hizo.
Msanii Cindy kutoka Uganda akikogonga nyoyo za mashabiki wake  katika ukumbi wa Mlimani City.
Beatrice Singano kutoka Airtel ambao walidhamini zawadi ya washindi mshindi wa 2 na 3 katika fainali za BSS 2010 akijiandaa kutangaza washindi walioshika nafasi hizo ambapo bahasha zenye majina ya washindi zikiwa mikononi mwa Mkurugenzi wa Bench Mark Production Madam Ritha Paulsen
Beatrice Singano, akimkabidhi Hundi ya Sh. milioni 10, kwa mshindi wa pili wa fainali za shindano hilo, James Martin anayeshuhudia tukio hilo ni Chief Judge Madam Ritha Paulsen. Washiriki wote walikabidhiwa na vyeti vy kushiriki vilivyotolewa na Kampuni ya Bench Mark.
Beatrice Singano akikabidhi hundi ya Shilingi milioni 5 kwa Mshindi wa tatu  Joseph Pyne.
Mariam Mohamed akionyesha furaha isiyo na kifani baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza.
eeeh Mungu..!!! asante kwa kusikia kilio changu na kutimiza ndoto zangu-Mariam Mohamed.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, akimkabidhi Hundi ya Sh. milioni 30, mshindi wa fainali za shindano la Bongo Star Search, Mariam Mohammed, baada ya kutangazwa mshindi. Katikati ni Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Production, Ritha Paulsen. Mbali na hundi hiyo Mariam alipata zawadi ya Bima ya afya kutoka AAR yenye thamani ya dola 150,000, Pesa taslim shilingi milioni 1 kutoka Mariedo Boutique na zawadi nyingine kibao.
Mariam baada ya kupokea hundi yake aliona asiondoke hivi hivi na kuwapa raha mashabiki wake waliompa ushindi huo na kuanza kucheza.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUSOMA HABARI ZILIZOPITA BOFYA NENO OLDER POSTS HAPO JUU ASANTE SANA KWA KUTEMBELEA NA KARIBU TENA