RAIS ZANZIBAR AAHIDI KUTEKELEZA AHADI ZA WAKATI WA KAMPENI
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
Wanawake
wa rika zote visiwani Zanzibar wametakiwa kutokuwa na hofu na
kuhakikishiwa kuwa ahadi zote zilizotolewa na rais wakati wa kampeni
zinazowahusu wao zitatekelezwa bila ya waiswasi.
Akizungumza
katika viwanja vya Kisonge rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amesisitiza kuwa ahadi zote
zitatekelezwa, ikiwemo sera ya wanawake na kundaa mpango maalum ili
kuhakikisha wanawake nao wanapata nafasi za juu za kuongoza.
Rais
huyo wa Zanzibar pia aliahidi kuwa serikali itahakikisha inapambana na
vitendo vilivyoshamiri vya udhalilishaji wanavyofanyiwa wanawake na
watoto.
Aidha
nao viongozi wa Umoja wa Wanawake akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja huo Bi.
Amina Nassor na Makamu Mwenyekiti Zanzibar Bi. Asha Bakari pamoja na
kumpongeza rais huyo pia walitoa wito kwa wanawake visiwani humo kuanza
kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment