MSHINDI WA BONGO STAR SEARCH APATIKANA
Mshindi wa shindano la Bongo Star Search 2010 ni Mariam
Mohamed(pichani).Hafla ya kumpata mshindi wa shindano hilo ilifanyikia
katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam mwishoni mwa wiki.
Jaji
Salama Jabir akitoa maoni kwa mshiriki. Salama amekuwa kivutio kikubwa
sana katika mashindano hayo kutokana na maoni anayotoa kwa washiriki
lakini mashabiki wanamchukulia kama ni mtu mwenye kukatisha tamaa na
kujilopekea tu la hasha, hiyo ni fani yake na anajua anachokifanya.
Nimekwambia kaa chini mimi ndio boss wako-Chief Judge Madam Ritha Paulsen akimkaripia kwa kumkalisha Jaji Master J baada ya kuwa mkaidi katika fainali hizo.
Mshiriki
Joseph Pyne ambaye alishika nafasi ya 3 katika fainali hizo aliteka
ukumbi mzima kwa kushangiliwa na kutunzwa pesa nyingi jukwaani kila
alipopanda na kufanya mashabiki wake kuacha midomo wazi kutokana na
kuimbia nyimbo ambazo mashabiki wanazikubali na kuzipenda.
Pichani
ni baadhi ya mashabiki wa Joseph Pyne wakihamaki kwa kutoamini
alichokuwa akiimba mshiriki huyo. Hebu tazama picha hii kwa umakini kila
shabiki anaonekana kuhamaki wenggine waliamua kusimama wakiona kwamba
wakika chini hawatofaidi vizuri..!!!
Wewe kuchukua milioni 30 usiku wa leo! i will shoot my self- Salama. Hayo
ni maoni ya Jaji Salama Jabir kwa Mshiriki Joseph Pyne kwa mtazamo wake
kwamba asipate kichwa kuona ukumbi nzima ukipiga nderemo kwa ajili
yake.
Vijana
wa THT wakitoa burudani wakati wa mapumziko mafupi huku washiriki wa
BSS 2010 wakisubiri kufanyiwa mchujo wa raundi ya pili katika fainali
hizo.
Mwanamuziki Mwasiti Almasi akitoa burudani katika fainali hizo.
TOP
5 ya BSS 2010 wakisubiri kuchujwa kuingia raundi ya pili katika fainali
hizo ambapo mshiriki Waiziri Salum (wa kwanza kulia) alienguliwa na
kuaga mashindano hayo lakini hakuondoka mikono mitupu alipata kitita cha
shilingi milioni 1 kutoka Bench Mark Production pamoja na Ofa ya
kurekodi nyimbo moja katika studio za MJ RECORDS pamoja na cheti cha
kushiriki mashindano hayo.
Mother House wa jumba la BSS 2010 naye alikuwepo akishuhudia watoto wake walibyokuwa wakitawala jukwaa katika fainali hizo.
Msanii Cindy kutoka Uganda akikogonga nyoyo za mashabiki wake katika ukumbi wa Mlimani City.
Beatrice
Singano kutoka Airtel ambao walidhamini zawadi ya washindi mshindi wa 2
na 3 katika fainali za BSS 2010 akijiandaa kutangaza washindi
walioshika nafasi hizo ambapo bahasha zenye majina ya washindi zikiwa
mikononi mwa Mkurugenzi wa Bench Mark Production Madam Ritha Paulsen
Beatrice Singano, akimkabidhi Hundi ya Sh. milioni 10, kwa mshindi wa
pili wa fainali za shindano hilo, James Martin anayeshuhudia tukio hilo
ni Chief Judge Madam Ritha Paulsen. Washiriki wote walikabidhiwa na
vyeti vy kushiriki vilivyotolewa na Kampuni ya Bench Mark.
Beatrice Singano akikabidhi hundi ya Shilingi milioni 5 kwa Mshindi wa tatu Joseph Pyne.
Mariam Mohamed akionyesha furaha isiyo na kifani baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza.
eeeh Mungu..!!! asante kwa kusikia kilio changu na kutimiza ndoto zangu-Mariam Mohamed.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, akimkabidhi Hundi ya Sh. milioni
30, mshindi wa fainali za shindano la Bongo Star Search, Mariam
Mohammed, baada ya kutangazwa mshindi. Katikati ni Mkurugenzi wa kampuni
ya Benchmark Production, Ritha Paulsen. Mbali na hundi hiyo Mariam
alipata zawadi ya Bima ya afya kutoka AAR yenye thamani ya dola 150,000,
Pesa taslim shilingi milioni 1 kutoka Mariedo Boutique na zawadi
nyingine kibao.
Mariam
baada ya kupokea hundi yake aliona asiondoke hivi hivi na kuwapa raha
mashabiki wake waliompa ushindi huo na kuanza kucheza.
0 comments:
Post a Comment