SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, December 28, 2010

TAMASHA DOGO LA ZIFF 31- Dec – 2010 NGOME KONGWE.
ZIFF LOGO
TAMASHA dogo la Zanzibar International Film Festival (ZIFF) ambalo limepewa jina la ZIFF Min ZIFF lipo tayari kufanyika baada ya kutangaza filamu zitakazoonyeshwa katika tamasha hilo, Mini-Festival itakayofanyika Ngome Kongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 31/12/2010 hadi 2/01/2011, itakua ni Tamasha dogo la siku 3 katika kutoa muamko kwa Tamasha kubwa la ZIFF lijalo (2-10 Julai, 2011).
Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania pekee yake (Swahili Films) ili kuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili litaonyesha filamu 8 za Kitanzania na filamu 2 bora kati ya hizo zitaenda kuoneshwa katika Tamasha kubwa la filamu Afrika – FESPACO huko Burkina Faso.
Filamu hizo ni Best Wife, Don’t Cry, Briefcase, Huba, Divorce, This is it, Nani, na Black Sunday, mbili kati ya filamu hizi ndiyo zitakazochaguliwa na kuingia kwenye maonyesho ya filamu makubwa Afrika – FESPACO nchini Burkina Faso.
Kama ilivyo ada ya Tamasha la Filamu la Nchi za Majahazi, kutakuwa pia na makundi ya muziki na wakati huu kundi zima la THT litafanya maonyesho kwa siku zote tatu, watakao kuwepo ni Mwasiti, Marlaw, Mataluma, Amin, Barnaba, Pipi, THT Dancers na wengineo. Kwa habari zaidi tembelea www.ziff.or.tz
Tamasha la ZIFF limekuwa na mafanikio makubwa kimataifa mwaka huu. Tarehe 3-5 Decemba ZIFF ilionyesha filamu zake huko Potsdam Ujerumani ambako mtengenezaji filamu Sajani Srivastava alionyesha filamu ya Tanzania “Nani” ambayo iliwafurahisha sana watazamaji.ZIFF pia ilionyesha filamu zake katika tamasha la Trinidad and Tobago na pia inatarajia kuonyesha filamu zake huko New york African Art Museum mwaka ujao.
Tayari matayarisho ya Tamasha la 14 yameanza na kwa sasa kuna uhakika wa kuwa na Workshop juu ya utengenezaji filamu itakayoendeshwa na Deustsche Welle ya ujerumani.
Kwa upande wa Muziki Clouds Entertainment wameingia mkataba na ZIFF kuendesha shughuli za muziki katika ZIFF.

0 comments:

Post a Comment