SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, December 23, 2010

Zimbabwe imetakiwa kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa wa amani
Rais Mugabe
Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi nyinginezo zimeitaka serikali ya umoja wa kitaifa ya Zimbabwe kufanya mabadiliko muhimu ili kuhakikisha uchaguzi wa mwaka ujao unafanyika kwa itibari, haki na amani. Taarifa iliyotolewa na nchi hizo sambamba na kukiri kupatikana kwa kiasi fulani maendeleo ya kiuchumi na masuala mengineyo, lakini imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuheshimiwa haki za binadamu, utawala wa sheria pamoja na kuheshimiwa makubaliano yaliyofikiwa na pande husika za nchi hiyo. Nchi hizo aidha zimesema kwamba, zitazishauri nchi jirani na Zimbabwe hasa Afrika Kusini kushirikiana na serikali ya Harare ili kutayarisha mazingira ya kufanyika uchaguzi huru, wa haki na wa amani. Rais Mugabe anasisitiza kufanyika uchaguzi mkuu katikati mwa mwaka ujao wa 2011 suala ambalo limeafikiwa pia na chama cha MDC kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment