Bashir asalimu amri kuhusu kura ya maoni
Omar al-Bashir
Rais wa marekani Barrack
Obama ametangaza kuwa swala la Sudan ni mojawepo wa ajenda kubwa ya
mashauri ya nchi za kigeni ya serikali yake.
Msemaji wa Ikulu ya White House Mike Hammer
amesema bwana Obama amekwishawaandikia barua viongozi wa Afrika
akiwataka kuunga mkono kura ya maoni kuhusu uhuru wa Sudan Kusini
itakayoandaliwa kwa njia ya amani.
Awali rais wa Sudan, Omar al-Bashir, alisema
Sudan Kaskazini itaimarisha sheria za kiislamu ikiwa Sudan kusini
itapiga kura ya kujipatia uhuru.
Bwana Bashir amesema kwamba ikiwa taifa hilo
litagawanywa, katiba ya Sudan itabadilishwa , Kiarabu itakuwa ndiyo
lugha ya pekee, dini ya pekee itakuwa ni Uislamu, na sharia ndiyo katiba
ya pekee itakayotumika nchini humo.
Mwandishi wa BBC mjini Khartoum amesema maneno
ya bwana Bashir yanawatia hofu raia wa Sudan Kusini ambao si waislamu na
ambao wanaishi Kaskazini.
Katika mkataba wa amani wa mwaka 2005
uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe, raia wa Sudan Kusini walilindwa
dhidi ya makali ya sharia.
0 comments:
Post a Comment