Iran imepuuzilia mbali vikwazo
vilivyowekewa nchi hiyo na baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa
sababu ya mpango wake wa nuklia.
Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinajad ametaja vikwazo
hivyo kama uzembe usio na maana yoyote na kusema kuwa thamani yake ni
tambara bovu lililotumika.
Vikwazo hivyo vipya vinaipiga marufuku Iran
kununua silaha nzito na kuweka sheria ngumu zaidi za kufanya biashara na
mabenki nchini humo.
Pia vimeongeza idadi ya viongozi wa nchi hiyo
waliopigwa marufuku kusafiri nje. Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa
vikwazo hivyo ni hafifu kuliko ilivyotarajiwa na mataifa ya magharibi
kutokana na shinikizo la Urusi na China. BBC SWAHILI
**********************
**********************
Watu 39 wauawa katika mlipuko uliotokea harusini nchini Afghanistan |
Watu wasipungua
39 wameuawa na 73 wengine kujeruhiwa baada ya kutokea mripuko katika
sherehe za harusi katika mkoa wa Kandahar wa kusini mwa Afghanisan.
Wengi wa waliouawa na kujeruhiwa katika mripuko huo ni wanawake. Mripuko huo umetokea wakati hadhirina walipokuwa wanakula chakula cha dhifa hiyo katika wilaya ya Arghanab iliyoko umbali wa karibu kilomita 30 kutoka mji wa Kandahar. Watoto wadogo 10 ni miongoni mwa waliojeruhiwa katika mripuko huo. Hadi tunapokea habari hii ilikuwa haijajulikana mripuko huo umesababishwa na kitu gani. Afisa mmoja wa hospitali kuu ya Kandahar amewaambia waandishi wa habari kuwa bado hawajajua ni watu wangapi hasa wameuawa na vile vile hawajui mripuko huo ulikuwa ni wa kujitoa muhanga, wa bomu au wa kitu gani kingine. Idadi ya wahanga wa mripuko huo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika tukio moja kwa miezi kadhaa sasa nchini Afghanistan. KISWAHILI RADIO.IRIB.IR |
0 comments:
Post a Comment