Akizungumza msemaji wa kundi hilo mapema leo ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,Hassan Umande alisema lengo la kuunda kundi hilo jipya ni kwa ajili ya kuendeleza sanaa na kuleta mabadiliko katika anga ya muziki wa kizazi kipya aka bongofleva hapa nchini.
"Mnajua waandishi, kiukweli kuna vikwazo vingi vilitokea mpaka tukaamua kujitenga ,yote hiyo kuepuka migongano ambayo kimsingi si ya lazima kwa sababu sisi wote ni vijana na tunatafuta maisha,kwa hiyo kwa sababu tumetengwa basi tumeamua kuunda kundi la watu sita"'amebainisha Hassani Umande.
Hassani amewataja wasanii watakaounda kundi hilo kuwa ni Athuman Yahya (A.Man), Juma Mbelwa (Juma Jazz), Karim Kaiman (Kakaman), Abdul Ally (Mzimu), Richard Shauri (Rich One) pamoja na David Mpangile (Daz-p).
Alisema mpaka sasa wamesharekodi nyimbo tatu ikiwemo, mapenzi kitu gani?, Poa tu pamoja na Mukide
Muda Wowote Kuanzia Sasa Watatoa Single Yao Mpya Itakayotambulisha Kundi Hili.
*********************************
Album inaitwa IVETA, itakuwa na jumla ya nyimbo 10,
baadhi ni IVETA, BINADAMU, MBALAMWEZI, SUBIRA, MGANGA, ROHO MBAYA,
NADHIFA nk.
Katika album hii atawashirikisha
BELLE 9, LINAH na JOSEFLY.. Lengo la kuwashirikisha wasanii wachache ni
kutaka kukionesha kipaji chake zaidi..
Studio zilizohusika kuipika album hii ni pamoja na TETEMESHA
RECORDZ (Kid bwoy), AB RECORDS (Amba), MUSIC LAB (Duke), MZUKA RECORDS
(Benja), A2P RECORDS (Sam Timba)
Tafadhali
tuipokee album yake itakapoingia sokoni.
0 comments:
Post a Comment