
Ule mtanange wa soka uliokuwa ukisubiriwa kwa shauku kubwa sana na mashabiki na wapenda kandanda wa Tanzania na nje ya nchi ya Tanzania, Leo umefikia kikomo baaada ya Brazil kuifunga Taifa Stars mabao 5 kwa 1 la kifutia jasho.
Mabao hayo kwa upande wa Brazil yalifungwa na wachezaji Robhino,Ramires na Kaka,kwa upande wa Taifa Stars bao hilo la kufutia machozi lilifungwa na mchezaji Aziz.
Ilikuwa ni mechi ya kirafiki Brazil wakiwa katika matayarisho kuelekea kwenye kombe la
Dunia Afrika ya Kusini 2010.
0 comments:
Post a Comment