
Shoo ilikuwa bab-kubwa katika swala zima la burudani kama unavyoona.

Lamar alipata tuzo ya mtayarisha bora wa muziki kwa mwaka 2008, na tuzo hiyo alikabidhiwa na Wakuvanga kutoka Komedy Show.

Meza ambayo alikuwa amekaa Sean Kingstone ilikuwa hii, alikuwa amekaa na wanyamezi wake.

Sean Kingstone akiongea na watanzania na akiwatambulisha watu waliokuja nao kabla ya kuitoa tuzo ya wimbo bora wa ragga

DJ wa Sean Kingstone akimtaja mshindi wa ragga ambaye alikuwa ni Bw. Misosi na wimbo wake wa Mungu yuko Bize.

Sean Kingstone akimkabidha zawadi Bw. Misosi.


Joh Makini alichukua tuzo ya wimbo bora wa Hip Hop

Chidi Benz alichukuwa tunzo ya msanii bora wa Hip Hop na alikabidhiwa na Sebbo

Hasheem Thabeet yeye alitoa tuzo kwa Video bora kwa mwaka 2008 ambayo
ilikwenda kwa CP na wimbo wake wa Problem hapa CP akizungumza machache
baada ya kuchukua tuzo.

Diamond akachukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka, jamaa alichukua tuzo 3.
AY akiongea mambo fulani kwa wageni rasmi akiwa amesindikizwa na Mwana FA na Prof Jay.
Na Dj Choka.
0 comments:
Post a Comment