
Hatimaye
Mwenyekiti wa kamati ya muda ya mahafali kwa mwaka huu Mh.Mustafa
Said(Matata)ametangaza rasmi sehemu itayofanyika mahafali kwa wahitimu
wa mwaka huu tarehe 26/6/2010 kama inavyoonekana pichani,sehemu hii inaitwa LEONIA RESORT.

Jamanii
panavutia kwa kweli kamati imeahidi makubwa ndani yake mnaombwa
wanajumuiya wote kujitokeza kwa wingi, kila mwanajumuiya anatakiwa
kuchangia kiasi cha 800 Rupees.

Wanaopenda kucheza kifupi kuogelea swimming kazi kwenu.

Sehemu kubwa sana makadirio kwa wanochezea maji wanasema humu wanaweza kuingia watu zaidi ya 160.

Sehemu ya mapumziko imetulia pia,kwa mbele yake kwa wale wanaopenda kujirusha na maji mtafurahi siku hiyo..

Mandhari tulivu ndani ya Leonia Resort kama yanavyoonekana.

Sehemu ya chakula hiyo mwanajumuiya usingoje kuadithiwa njoo ujionee mwenyewe.

Baadhi ya viwanja vya michezo,viwanja vyote vya michezo vipo ndani ya Leonia Resort.

Hawa
ni baadhi ya wanakamati waliokwenda kukagua,mbele kabisa
Bw.Daniel Masimbusi,anaefuata Bi.Neema,nyuma mbele Bw.Dunstan na
anaefuata Bi.Joharia Nkya.

Wakiwa ndani kwa ukaguzi zaidi.

Bi.Neema na Bi.Joharia wakipata kumbukumbu ya pamoja baada ya kumaliza ukaguzi huo.
Imetayarishwa na kamati TSAH 2010.
0 comments:
Post a Comment