SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, May 16, 2010

Miss Dar Inter College Yalamba Mpunga Mnene Leo


Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari waliofika leo katika Hoteli ya Movenpic wakati wa akitangaza udhamini wake wa Mil. 12 kwa ajili ya shindano la Miss Dar Inter College Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akikabidhi Hundi yenye Thamani ya shilingi Mil. 12 kwa Mratibu wa Shindano la Miss Dar Inter College,Silas Michael huku warembo washiriki wakishuhudiaa.
warembo wakilamba picha ya pamoja na Mama Rahma Al Kharoos
mzee wa Mtaa Kwa Mtaa akiwa na Mratibu wa Miss Dar Inter College,Silas Michael katika mnuso ulioandaliwa na Mdhamini wa shindano hilo katika Hotel ya Movenpic mchana huu.
warembo wakijisevia mahanjumati
Othman akipiga mnuso pamoja na warembo
msosi taimu yaani ni full mzuka.

*******************************

KAMPUNI ya RBP & INDUSTRIAL TECHNOLOGY TANZANIA LIMITED ya jijini Dar es Salaam leo imetangaza kudhamini shindano la Miss Dar Inter College na imeweza kutoa kiasi cha shilingi milioni 12 kwa ajili ya zawadi za warembo wanaowania taji hilo litakalofanyika May 27 kwenye klabu ya kimataifa ya Bilicanas jijini Dar es Salaam.

Warembo watakaoshiriki shindano hilo ni kutoka vyuo vya mbali mbali vya elimu ya juu vya jijini Dar vikiwemo CBE, IFM, DSJ, TSJ, ISW.

Akiongea na Waandishi wa habari waliofika katika mkutano uliofanyika leo katika Hoteli ya Movenpic,Rais wa Kampuni hiyo ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY TANZANIA LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos alisema.”Kampuni yangu ya RBP ni ya kizalendo na imeona vyema kuwasaidia warembo hawa ambao ni wasomi na pia ni taifa la kesho na ambao wataweza kuleta maendeleo katika nchi yetu kupitia fani hiyo ya urembo”.

Aliendelea kusema “Ninawapa msaada huu Warembo hawa kama wanangu na hivyo kama Mama ninaejali familia na watoto kwa ujumla nimeona leo niweze kuwasaidia katika kufanikisha kupatikana kwa zawadi zitakazoweza kuwanufahisha maishani mwao.”

Msaada huo ni mwendelezo tu wa kusaidia na kuinua vipaji vya wasichana hapa nchini ambapo juzi tu Mdhamini huyo aliweza kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa timu ya taifa ya wanawake ‘TWIGA STARS’ ambayo inajiandaa na kucheza michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake.

Twiga itacheza na timu ya taifa ya Elitrea May 23 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo unaotazamiwa kuwa na upinzani mkali.

Kwakumalizia Mama Al Kharoos aliwahusia warembo hao kwa kuwataka waepukane na vishawishi na mambo yasiyofaa katika Jamii pia wawe na tabia njema waapo majumbani mwao. Kwani kujiheshimu kwao ndiko kutakapo wapatia heshima katika sehemu yoyote ile watakayokuwepo.

RAHMA AL KHAROOS
President – RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY 

Muandishi: Othman Michuzi

0 comments:

Post a Comment