BANGKOK
Waziri Mkuu wa Thailand, Abhisit Vejjajiva ametetea hatua zilizochukuliwa na jeshi la nchi hiyo hapo jana dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali. Akizungumza katika televisheni, Bwana Vejjajiva alisema hatua hiyo ya jeshi ni njia pekee ya kumaliza vurugu zinazofanywa na waandamanaji hao wanaojiita ''mashati mekundu''.
Imeelezwa kuwa vikosi vya jeshi la Thailand vilifyatua risasi za moto na zile za mpira kwa waandamanaji hao waliokuwa wakirusha mabomu ya kutengenezwa hapo kwa hapo pamoja na mawe.
Mashirika ya misaada yamesema kuwa kiasi watu 24 wameuawa na wengine 200 wamejeruhiwa tangu wanajeshi wa Thailand waizuie wilaya ya kibiashara mjini Bangkok, siku ya Ijumaa. Aidha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amewataka viongozi wa serikali ya Thailand na waandamanaji hao kutatua mzozo wao kwa njia ya mazungumzo.
Habari na Deutsche Welle

0 comments:
Post a Comment