Takwimu mpya zilizotolewa na
Umoja wa Mataifa zimeonyesha kuenea kwa virusi vya HIV miongoni mwa
vijana kwenye nchi zilizoathirika zaidi na ukimwi, hasa barani Afrika
zimepungua.
Katika ripoti hiyo, UNAids imesema idadi ya watu
wenye virusi vya HIV imepungua hadi kufikia asilimia 25 kutokana na
vijana kati ya miaka 15-24 kubadili tabia zao za kujamiiana.
Ripoti hiyo imesema matokeo hayo ni kutokana na
kampeni za kuzuia kuenea kwa virusi vya ukimwi.
Lakini Umoja wa Mataifa umesema umeongezeka
Uganda, nchi iliyosifiwa kwa kupambana na ugonjwa huo.
Kulingana na umoja huo, vijana milioni tano
wanaishi na virusi vya ukimwi duniani, na hivyo kuwepo na maambukizi
mapya kwa asilimia 40.
' Onyo'
Kampeni kali ya Uganda dhidi ya HIV/Aids
ilisaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya ukimwi -iliyofikia
aslimia 30 katika miaka ya 1990.
Mkurugenzi mkuu wa UNAids Michel Sidibe
ameiambia BBC, " Baada ya maambukizi hayo kupungua na kutolewa kwa
matibabu, wengi wao hawakuwa na wasiwasi tena kama ilivyo mwanzo katika
mipango ya kuzuia."
"Kwahiyo matokeo tunayoyashuhudia leo Uganda ni
jambo linalotakiwa kututisha-hasa maendeleo yake na namna ya kuhakikisha
idadi haiongezeki ambayo huenda kuridhika ndio kumesababisha hilo."
Alisema, hata hivyo takwimu nyingine ni ishara
nzuri ya mabadiliko kwani vijana barani Afrika wamekuwa makini zaidi na
afya zao.
" Kwangu mimi, hiyo ni hatua kubwa sana katika
mipango yetu ya kuzuia." bbc swahili.
0 comments:
Post a Comment