Bi. Itika Kasambala akiwa katika moja ya vyumba vya
habari baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi
Bi Itika kasambala akiwa katika picha tofauti jijini
Dar es Salaam baada ya kuelezea sakata lake na Naibu Waziri wa kazi,
Ajira na Maendeleo ya Vijana
Baadhi ya nakala za malada ya kesi hiyo
iliyofunguliwa mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi na
Bi. Itika Kasambala dhidi ya Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo
ya Vijana.
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana,
Dkt Mahongoro Mahanga akitoka katika chumba cha mahakama ya kazi, Tume
ya Usuluhishi na Upatanishi wiki iliyopita siku ya Jumanne baada ya
kusomewa mashtaka yake ya kumfanyisha kazi PS wake (Private Secretary)
Bi, Itika Kasambala katika ofisi yake ya Bunge kwa muda wa miaka kumi
bila mkataba na kusitisha kazi yake na kisha kulipa mafao ya laki mbili
tu
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
akishuka katika kazi za mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi
wiki iliyopita siku ya Jumanne jijini Dar es Salaam
----
Na. Mwandishi wetu
NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana,
Dkt Makongoro Mahanga ameingia kwenye kashfa nzito ya kuvunja sheria
za kazi nchini kwa kumfanyisha kazi msaidizi wake (PS) wa ofisi yake
Bunge kwa miaka kumi bila mkataba na kumlipa fedha taslimu shilingi
laki mbili tu (200,000) kama mafao.
Naibu Waziri, Mahanga anakuwa kiongozi wa kwanza kuingia
kwenye kashfa akiwa madarakani tena kwenye swala la ajira wakati yeye
mwenyewe ni waziri mwenye dhamana na maswala ya ajira na haki za wafanyakazi
nchini chanzo chetu kimeelezwa.
Kwa mujibu wa sheria kazi na mahusiano kazini, Naibu
Waziri amekiuka kifungu cha 3 cha sheria ya Taasisi za kazi za mwaka
2004 na pia amekiuka sehemu ya tatu ya viwango vya ajira na sehemu ndogo
A kwa kushidwa kuandika mkataba kwa mujibu wa kifungu cha 14 ibara ya
kwanza kama sheria ya kazi na mahusiano kazini inavyotaka.
Katika kifungu hicho cha 14 ibara ya kwanza kinasema
mkataba utakuwa wa kipindi cha muda usiotajwa, mkataba wa kazi maalumu
na mkataba unatakiwa kuwa wa maandishi ambapo vyote Mhe Naibu Waziri
hakufanya.
Ibara ya 15 kifungu cha.-(1) kinasema kwa kuzingatia
masharti ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu cha 19, mwajiri anatakiwa
kumpa mfanyakazi, wakati mfanyakazi anapoanza kazi, taarifa zifuatazo
kwa maandishi, jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi;
mahali alipoajiriwa; kazi zake; tarehe ya kuanza; muundo na muda wa
mkataba; kituo cha kazi; masaa ya kazi; ujira na njia ya ukokotoaji
wake, na taarifa za mafao mengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni
jijini Dar es Salaam, Bi. Itika Kasambala (31) anasema alianza kazi
kwa Mbunge huyo wa Segerea na Naibu Waziri wa kazi Dkt. Mahanga, mwaka
2003 kama PS (Personal Secretary) kwa makubaliano ya kumpa mshahara
wa shilingi 120,000 kwa mwezi lakini alianza kumlipa shilingi 50,000
tu.
“aliniambia kwamba nianze kazi kwanza baadaye
atanipa mkataba wa ajira na kunilipa mafao ya hifadhi ya jamii na matibabu
lakini baada ya miaka kumi ananitumia sms akiwa Dodoma kwamba kazi basi
sikuhitaji tena,” Kasambala alisema.
Amesema kwamba Mbunge huyo alimtumia sms akiwa kwenye
vikao vya bunge mjini dodoma mwaka jana mwezi wa sita akimjulisha kwamba
ajira yake imeshafika kikomo kwa sababu hana uwezo tena wa kumlipa mshahara
na mahitaji mengine ya kiofisi.
Kasambala aliendelea kusema kwamba mara ya kwanza
wakati anaanza kazi mwezi wa tano mwaka 2003 baada ya msaidizi wa ofisi
ya mbunge Mahanga kuacha kazi na ndipo alipotafutwa yeye na walikwenda
kuelewana kwa malipo ya 120,000 kwa mwezi.
Alisisitiza kwamba mara baada ya kuanza kazi kwa ofisi
ya mbunge alikuwa analipa pesa kupitia mkononi na baadaye tigo pesa
na baada ya muda akawa anachukua pesa yake ya mshahara toka katika manisapaa
ya Ilala kama posho ya Mhe Mahanga kama diwani kila mwezi.
Dada huyo kwa mshangao baada ya mahojiano ya muda
mrefu alikiri kwamba Mhe Mahanga alikuwa na nia ya dhati kuanzisha mahusiano
ya kimapenzi na kumtaka aende Dodoma lakini alikataa kufanya masharti
hayo.
“mwaka juzi baada ya kuonyesha nia ya kunitaka kimapenzi
alinipigia simu akitaka niende Dodoma bungeni kwa mazungumzo zaidi kama
msaidizi wake lakini nilikataa,’ aliongeza Kasambala.
Amesema tangu aanze kazi kwa Mhe Mahanga hakuwa anatoa
huduma zozote kama matibabu au fedha kwa ajili ya sikukuu ilikuwa ni
mshahara tu wa 120,000 kwa mwezi lakini kila akimfuata ili waandikishiane
mkataba alikuwa akizungumsha bila sababu za msingi.
Bi. Kasambala aliongeza kuwa amefanya kazi Mhe Mahanga
tangu akiwa mbunge wa Ukonga na baadaye Segerea lakini ameshidwa kuheshimu
sheria za ajira na taratibu za kazi wakati yeye mwenyewe ni waziri mwenye
dhamana ya ajira kwa watanzania.
Amesema mwaka jana tarehe 14/09/2013 alimtumia kwa
Tigopesa kiasi cha shilingi za Tanzania 200,000 kama mafao yake baada
ya kufanya kazi kwa takribani miaka 10 kama Msaidizi wake wa Ofisi ya
Mbunge.
Amesema kwamba aliamua kwenda Chama cha Wafanyakazi
wa Hifadhi, Mahoteli, Majumbani na Kazi Nyingine (CHODAWU) kwa msaada
wa ksiheria ba baada ya kukutanishwa bado Mhe Mahanga akawa mgumu kukubaliana
kiungwana mpaka ikawalazimu kwenda mahakani Tume ya Usuluhishi na Upatanishi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakili wa
Kasambala, Nyaisa Godwin alisema kuwa kesi imefunguliwa mahakama ya
kazi wiki iliyopita siku ya Jumanne, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi
kesi namba CMA/DSM/ILA/R.711/13.
Wakili Nyaisa alisisitiza kwamba Naibu Waziri aliiambia
mahakama kwamba Dada Kasambala alikuja kufanya kazi kwake kama mwanafunzi
wa chuo kwenye mazoezi lakini alishidwa kuithibitishia mahakama kwa
ushawishi wa barua ya (field to chuoni).
“tulishagazwa na majibu ya waziri kwamba dada huyo
alikuwa field, na nilimuuliza field ya miaka kumi? Alishidwa kutoa jibu
mbele ya mpatanishi (Arbitrator),” amesema Nyaisa.
Nyaisa aliendelea kusema kutokana na matatizo ya kuachishwa
kazi ghafla bila taratibu dada huyo amepata maradhi ya presha, vidondo
vya tumbo na maradhi mengine baada ya kufanya kazi kwa Mhe Mbunge kwa
miaka kumi bila matibabu wala kulipiwa mifuko ya hifadhi za jamii.
Wakili Nyaisa aliongeza kwamba kesi hiyo ya aina yake
dhidi ya Naibu Waziri wa Kazi itasomwa tena tarehe 13/02/2014 katika
Tume ya Usuluhisho na Upatanishi.
Juhudi za kumtafuta, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na
Maendeleo ya Vijana, Dkt. Mahanga hazikuzaa matunda baada ya simu yake
ya kiganjani kushidwa kupatikana kwa muda mrefu alipotafutwa kwa ajili
ya kutoa ufafanuzi.
CHANZO: H@KI NGOWI
CHANZO: H@KI NGOWI
0 comments:
Post a Comment