SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, January 18, 2014

NEW YORK YAJADILI UFANISI WA SHERIA ZINAZODHIBITI BIASHARA YA PEMBE ZA TEMBO

Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira ya Bunge la New York, Bw. Robert K. Sweeney akiongoza mkutano ( public hearing) aliouandaa kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu ufanisi wa sheria na kanuni zinazodhiti biashara ya pembe za tembo katika New York, mkutano huo ulifanyika siku ya Alhamis. New York ndiyo inayoongoza katika Marekani kwa kuwa kituo cha Biashara ya pembe za tembo na biadhaa zake katika mwaka 2012 pembe za tembo zenye thamani ya dola milioni mbili zilikamatwa.
Muwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza katika mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine alielezea jitihada zinazofanywa na serikali katika kudhibiti ujangili na biashara haramu ya pembe za tembo.
Bw. William C. Woody ( mwenye tai ya njano) Naibu Mkurugenzi kutoka Ofisi inayosimamia sheria akiwa na Bw. Richard G. Ruggiero Mkuu wa Kitengo cha Afrika, Uhusiano wa Kimataifa , huduma za Samaki na Wanyamapori nchini Marekani. Wakitoa ushuhuda wao kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika udhibiti na usimamizi wa sheria zinahusu biashara ya pembe za tembo na wanyama wengine walio katika hatari ya kutoweka.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia majadiliano hayo ambayo pia yaliwahusisha wataalam kutoka Asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na hifadhi ya mazingira na mali asili.
Balozi Tuvako Manongi akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira, Bw. Robert K Sweeney ( Mb).

Na Mwandishi Maalum

Wakati Serikali ya Tanzania ikijipanga kwa utekelezaji wa awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza Ujangili, Bunge la New York, nchini Marekani, kupitia Kamati yake ya Hifadhi ya Mazingira linajipanga kuangalia namna ya kuboresha ufanisi wa sheria na kanuni zinazolinda na kudhibiti biashara ya pembe za Tembo na wanyama wengine.

Katika kutekeleza azima hiyo, jana alhamisi, hapa New York, Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira Robert K. Sweeney(Mb) aliitisha mkutano ( public hearing) uliokuwa na lengo la kusikiliza michango na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, michango ambayo kwa namna moja ama nyingine itachangia katika uboreshaji wa sheria na sera zilizopo hivi sasa.

Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, alikuwa miongoni mwa waalikwa waliopewa fursa ya siyo tu, kutoa ushuhuda wa ukubwa wa tatizo la ujangili na adhari zake. Lakini pia kuelezea nini mamlaka husika zinafanya kukabiliana na tatizo hilo na kutoa ushauri na mapendekezo ya hatua zaidi za kukabiliana na changamoto hiyo.

Pamoja na kuwasilisha ushuhuda wake na hatua zinazochuliwa na serikali , Balozi Manongi pia alijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na Mwenyekiti wa Kamati na wajumbe wengine.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira, Robert Sweeney alisema. Tembo wa Afrika ambao ni urithi wa dunia na muhimu kwa ustawi wa mwanadamu wamo hatarini kutoweka kama hatua madhubuti zaidi hazitachukuliwa.

Akatahadharisha kuwa uwindaji haramu wa tembo kwaajili ya pembe zao siyo tu kwamba umekidhiri na kuongezeka badala ya kupungua, lakini pia hivi sasa mitandao ya mbalimbali ya uhalifu na ugaidi inajiingiza kwa kasi katika eneo hilo.

“ Hali ni mbaya, mauaji ya tembo yanaongezeka, tunahitaji kuchukua hatua zaidi na ndio maana nimeitisha mkutano huu ili kuangalianamna gani sheria na kanuni zetu zilizopo zitaweza kuwa na ufanisi zaidi katika kudhibiti biashara ya meno ya tembo” akasema Mwenyekiti.

Akabinisha kwamba katika New York biashara ya meno ya tembo inadhibitiwa kupitia sheria na kanuni mbalimbali lakini pamoja na sheria hizo, bado New York inaongoza katika Marekani kwa kuwa kituo cha biashara ya pembe za tembo.

Akatoa mfano kwa kueleza kuwa katika mwaka 2012, pembe za tembo zenye dhamani ya dola 2 milioni ambazo ziliingia New Yor kwa njia zisizo halali zilikamatwa na kutekezwa. Na kwamba tatizoni kubwa.

0 comments:

Post a Comment