SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 1, 2013

WATANZAIA WATINGISHA MJINI KOLONI UJERUMANI


Wageni wakijichagulia bidhaa za Tanzania wakati wa sherehe hizo.

Dada Tabia Mwanjelwa (mwenye) gitaa akiwa na wasanii wenzie jukwaani.
Maana ya Muungano yakubalika na watoto wa kimataifa! Ngoma Inogile!.

Msanii John Gambula na Tadeo Simon, wakiwa na watoto jukwaani.

Wasanii wa kikundi cha Wabantu wakiipeperusha TZ.

Dada Tabia Mwanjelwa (mwenye gitaa) akiwa na wasanii wenzie jukwaani.
Siku ya Jumamosi 27.04.2013 Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani, chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno "MUUNGANO" lina maana kamili kwa maisha ya  Mtanzania na binadamu wengine.
Sherehe hizo zilizowakusanya Watanzania na marafiki waTanzania kutoka kila kona  ya Ujerumani, ziliutingisha mji wa Koloni katika usiku usio kwisha wa kusherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Ali Siwa, Naibu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikuwa mstari wa mbele akiwaongoza Watanzania katika Muungano Day.
Wasanii mbalimbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tanzania. Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Mfundo na kamati yake wameahidi kufanya mambo makubwa na kuitangaza Tanzania kwa hali na mali chini  ya  Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU).

0 comments:

Post a Comment