SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, August 1, 2014

MABOMBA YA GESI YALIPUKA NA KUUA 24 NCHINI TAIWAN


Mfululizo wa milipuko ya gesi kusini mwa Taiwan katika mji wa Kaohsiung imeuwa watu 24 na kujeruhi watu 270.



Milipuko hiyo imetikisa wilaya ya mji huo ya Cianjhen, magari yaliyorushwa yamesambaa na barabara zimepasuka na kuwa na mitaro.


Chanzo halisi cha kuvuja kwa gasi hakijafahamika, lakini imefahamika kuwa milipuko hiyo imetokana na kupasuka kwa mabomba ya gesi.
MMMMMM
 Moto uliozuka baada ya milipuko ya gesi nchini Taiwan. 
WATU 22 wamefariki dunia huku 270 wakijeruhiwa baada ya milipuko kadhaa iliyosababishwa na kuvuja kwa gasi kutokea katika jiji la Kaohsiung nchini Taiwan jana usiku. Mlipuko huo uliosababisha moto mkubwa uliopindua magari, kuharibu barabara na baadhi ya majengo.
Majeruhi makitolewa eneo la mlipuko.
 Moto mkubwa ukiendelea kuwaka mtaa wa Kaohsiung nchini Taiwan
  Magari, barabara vikiwa vimeharibiwa na milipuko hiyo.

Maafa zaidi yaliyosababishwa na milipuko hiyo.

0 comments:

Post a Comment